
MKOA wa Dodoma kumepangwa kujengwa uwanja mpya wa michezo wa kisasa kwa gharama ya Sh. 358 bilioni, sawa na dola za Marekani 140 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 32,000 kwa wakati mmoja na utatandazwa nyasi bandia za kisasa zinazokidhi viwango vya kimataifa.
Mradi huu unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya vijana na wakazi 3,500 wa mkoa wa Dodoma, moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mkoa huo.
Kwa mujibu wa wataalamu wa michezo, uwepo wa uwanja huo utakuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa sekta ya michezo nchini, sambamba na kuvutia mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Aidha, mradi huo unatarajiwa kuinua maisha ya wananchi kupitia fursa mpya za kiuchumi zitakazotokana na shughuli za michezo, biashara ndogo ndogo na sekta ya huduma.
Wadau wa michezo wamesema ujenzi wa uwanja huu unadhihirisha dhamira ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza michezo, kuendeleza vipaji na kulifanya jiji la Dodoma kuwa kitovu cha matukio makubwa ya michezo nchini.
ZINAZOFANANA
Wananchi kuanza utetezi wa ubingwa NBCL leo
Uwanja wa Mkapa wakarabatiwa kwa Sh. 31 bilioni
Europa League kukupeleka moja kwa moja kwenye ushindi wa Meridianbet.