
Jair Bolsonaro
MAHAKAMA nchini Brazil imemhukumu kifungo cha miaka 27 na miezi mitatu jela aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Jair Bolsonaro, baada ya kumkuta na hatia ya kupanga njama za kupindua Serikali. Inaripoti Mitandao ya Kijamii … (endelea).
Uamuzi uliopitishwa na Majaji wanne kati ya watano waliosikiliza Kesi, umeonesha baada ya kushindwa katika Uchaguzi, Bolsonaro aliandaa mikakati ya kumuua mpinzani wake, Rais Luiz Inácio Lula da Silva.
Mawakili wa kiongozi huyo wamewasilisha Rufaa kupinga kesi hiyo pamoja na kutaka awekwe chini ya ulinzi akiwa nyumbani kwake badala ya kupelekwa Gerezani.
ZINAZOFANANA
Félicien Kabuga kurejeshwa Rwanda?
Mke wa Rais Ivory Coast ajitosa kwenye mbio za urais
Mike Tyson kurudi ulingoni na Mayweather 2026