
MKEWA wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Simone Gbagbo (76), amejitosa katika kinyang’anyiro cha urais. Inaripoti Mitandao ya Kimatiafa … (endelea).
Jina la Simone, limeonekana katika orodha ya wagombea watano walioidhinishwa rasmi kugombea nafasi hiyo, katika uchaguzi wa mwezi ujao. Anatarajiwa kukabiliana na rais wa sasa, Alassane Ouattara (83), anayetetea wadhifa wake.
Outtara alichukua mamlaka ya urais baada ya kumshinda Laurent Gbagbo – mume wa Simone – aliyekamatwa kwenye chumba cha kulala cha rais wakati wa mzozo ulioikumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa 2010.
Rais huyo wa zamani ameondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho, kama ilivyo kwa aliyekuwa waziri mkuu Pascal Affi N’Guessan na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Credit Suisse Tidjane Thiam.
Kuondolewa kwao kumeibua wasiwasi kuhusu uhalali wa uchaguzi wa 25 Oktoba na kuzua hofu ya kukosekana kwa utulivu.
ZINAZOFANANA
Mike Tyson kurudi ulingoni na Mayweather 2026
Rais mstaafu Peru ahukumiwa miaka 13 jela
Maporomoko yaua 1,000 Sudan