
MUONGOZAJI wa filamu nchini Tanzania, Adarus Walii ambaye pia ni msanii, ameingiza sokoni filamu yake inayojulikana kwa jina la ‘Mke wa Mama’ hivi karibuni katika mitandao mbalimbali ya kijamii ukiwemo ‘YouTube’. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam .. (endelea).
Walii amewahi kutamba na filamu mbalimbali kama ‘Muuza Genge’, ‘Aisha’, ‘Namtaka Mwanangu’, ‘Bondo DSM’, ‘Slay Queens’ na ‘Mapenzi na Muziki ambazo zilimtangaza vizuri katika medani ya Bongomuvi hapa nchini.
Akizungumza Dar es Salaam, Walii amesema filamu hiyo ina mafundisho makubwa katika jamii hasa ukizingatia wasanii walioshiriki wameitendea haki filamu hiyo.
“Filamu hii inamuhusu kijana anayetambulika kwa jina la Walii ambaye alipata changamoto zilizosababisha mama yake kuamua kumuolea mke kwa niaba yake,” amesema Walii na kuongeza.
“Kitendo hicho ndio kikaongeza changamoto kwa Walii na kusababisha taharuki katika jamii, ni kisa ambacho kipo katika maisha ya kila siku”.
Akizungumzia utofauti wa filamu hiyo na nyinginezo, Walii amesema:” Tofauti ni mkubwa ukianzia katika ujumbe uliopo si ule uliozoeleka, kwani watu wengi wanapoona mtu anachelewa kutoa maamuzi huamua kutoa wao bila kujua athari za huko, hivyo wanajikuta wanakosa njia mbadala ya kutatua changamoto zitakazotokea kutokana na maamuzi waliyofanya bila kujipanga.
Ameongeza filamu hiyo imehusisha wasanii chipukizi kwa kiasi kikubwa na kiukweli wamefanya vizuri sana katika kazi hiyo.
Amewataka watanzania na mashabiki zake kwa ujumla kusapoti maudhui ya filamu hiyo bila kujali majina ya wasanii waliocheza zaidi waangalie ujumbe uliopo katika filamu hisuka.
ZINAZOFANANA
Thamani ya klabu ya Yanga yafikia Sh. 100 Bilioni
Tulikataa Bilioni 5 kumuuza Mzize – Hersi
Wikendi ya kutusua na Meridianbet hapa