September 7, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Thamani ya klabu ya Yanga yafikia Sh. 100 Bilioni

 

MWENYEKITI wa kamati ya mabadiliko ya uwendeshaji wa klabu ya Yanga Wakili Alex Mgongolwa amesema kuwa thamani ya klabu hiyo kwa Sasa ni shilingi 100 Bilioni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Wakili Mgongolwa ameyasema hayo, wakati akisoma ripoti ya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu katika mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama, uliofanyika kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa, kupitia thamani hiyo Yanga inaweza kuendelea na mchakato wa mabadiliko kwa kuzingatia Sheria na katiba kwenye soko la hisa.

“Thamani ya klabu ya Yanga SC ni shilingi Bilioni 100, klabu ya Yanga Sasa inaweza kuendelea na mchakato wa mabadiliko kwa kuzingatia matakwa ya katiba na sheria za soko la hisa,” alisema Wakili Mgongolwa.

About The Author

error: Content is protected !!