
RAIS wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji, ametangaza kuachia rasmi nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ili kutoa nafasi kwa uongozi wake karibu zaidi na ushirikiwa moja kwa moja katika shughuli za kila siku za klabu. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Katika taarifa rasmi, Dewji ameeleza kuwa kutokana na majukumu mengine ya kibiashara na ukweli kwamba mara nyingi amekuwa mbali na shughuli za klabu, imekuwa busara kumpisha kiongozi mwenye muda na upatikanaji wa karibu kuongoza Bodi ya Wakurugenzi.
“Nitaendelea kuwa Mwekezaji na Rais wa Simba SC, lakini nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi sasa ninakabidhi kwa kiongozi mwingine,” alisema Dweji.
Kwa mamlaka aliyopewa chini ya Katiba na Kanuni za Kampuni(MEMARTS) ya Simba Sports Club Company Ltd na anayo haki ya kuteua viongozi wa Bodi.
Kwa kutumia Mamlaka hayi Mohamed Dewji ametangaza kumteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC.
Aidha, Rais Dewji ametangaza pia uteuzi wa wajumbe wa Bodi Hussein Kitta Mjumbe wa Bodi, Azim Dewji-Mjumbe wa Bodi, Rashid Shangazi- Mjumbe wa Bodi, Swedi Mkwabi, Mjumbe wa Bodi, Zuly Chandoo, Mjumbe wa Bodi, George Ruhango, Mjumbe wa Bodi Barbara Gonzalez
ZINAZOFANANA
Mechi za kufuzu WC Ulaya kukupatia mkwanja leo
Rekodi mpya za usajili na Meridianbet hizi hapa
Bashiri mapema anayeshuka daraja EPL 2025/26