
KAMPUNI ya KoBold Metals ya nchini Marekani inayoungwa mkono na Bill Gates na Jeff Bezos, imepata leseni saba za uchimbaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Leseni hizo zinajumuisha eneo la Manono, linalojulikana kwa hifadhi kubwa ya lithium pamoja na Malemba Nkulu.
Leseni hizo zinaruhusu eneo lenye ukubwa wa kilomita 4,500 huko Manono tayari linajulikana kuwa ni mojawapo ya mashapo makubwa ya lithium duniani.
DRC inazalisha takribani asilimia 70 ya kolbati duniani inalenga kupanua nafasi yake kama mshiriki mkuu katika mpito wa nishati safi.
Shinikizo limewekwa kwenye uchunguzi wa madini ya lithium, ingawa leseni zinaruhusu pia uchunguzi wa madini kama vile coltan, madini adimu, bati na dhahabu.
Makubaliano ya awali kati ya KoBold na serikali ya DRC yalifikiwa Julai 2025, Agosti 2025: Leseni saba zimeidhinishwa (4 Manono, 3 Malemba Nkulu) na kutoa haki ya kuanza mpango mkubwa wa uchunguzi.
KoBold inatumia akili mnemba (AI) kuchambua data za kijiolojia na kuendesha uchunguzi kwa ufanisi zaidi.
ZINAZOFANANA
Maporomoko yaua 1,000 Sudan
UN walia kuzorota haki za binadamu Burundi
Tetemeko laua 800 Afghanistan, Pakistan