September 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

UN walia kuzorota haki za binadamu Burundi

 

WATAALAM wa Umoja wa Mataifa (UN), wameeleza wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi, hususani mashambulizi dhidi ya wapinzani wa kisiasa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea). 

Wamesema vitendo hivyo vinafanywa na maofisa wa usalama au watu wanaoshirikiana na mamlaka bila wahusika kuwajibishwa.
Kati ya Januari 2024 na Mei 2025, mashirika ya kiraia yameripoti visa 200 vya unyanyasaji wa kijinsia (ikiwemo ubakaji wa watoto),watu 58 kupotezwa, 62 kuteswa, 892 kuzuiliwa kinyume cha sheria na 605 kuuawa kwa kupanga.

Wataalamu hao wamesema ukiukwaji huu umetumika kuwatisha raia wakati wa uchaguzi ambapo chama tawala CND-FDD kilishinda kwa asilimia 96 ya kura na kupata viti vyote 100 bungeni katika Uchaguzi wa Juni 2025.

Licha ya ahadi za Rais Evariste Ndayishimiye za mageuzi ya haki tangu aingie madarakani mwaka2020 lakini mambo yanaonyesha kuwa haki za binadamu zimezidi kuzorota.

About The Author

error: Content is protected !!