UINGEREZA imefunga kwa muda ubalozi wake mjini Cairo nchini Misri, baada ya mamlaka ya nchi hiyo, kuondoa vizuizi vya usalama nje ya jengo hilo,huku kukiwa na mzozo wa kidiplomasia kuhusu kukamatwa kwa mwanaharakati. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza, ilisema jengo lake kuu la ubalozi katika Wilaya ya Mji Mkuu wa Garden City litaendelea kufungwa wakati athari za mabadiliko zikikaguliwa,lakini ikaongeza ubalozi huo ukiendelea kufanya kazi.
Uamuzi huo unafuatia kuongezeka kwa wito nchini humo wa kulipiza kisasi jinsi Uingereza ilivyoshughulikia maandamano mjini London, ripoti zinasema.
Wiki iliyopita,mwanaharakati maarufu wa serikali ya Misri alikamatwa na baadaye kuachiliwa baada ya kukabiliana na waandamanaji nje ya ubalozi wa Misri nchini Uingereza.
ZINAZOFANANA
Umoja wa Afrika: Uchaguzi wa Tanzania ulivurugwa
Mambo matano makubwa kuhusu Raila
Raila Odinga alikuwa mwanaharakati wa demokrasia – Barack Obama