
Benjamin Netanyahu
MAELFU kwa maelfu ya waandamanaji wameingia mitaani mjini Tel Aviv, Jumamosi jioni, kupinga mpango wa Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa Israel, kuzidisha vita vya Gaza na kutaka kulikalia eneo hilo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Vita vya Gaze vimedumu kwa takriban miaka miwili sasa; waandamanaji wanatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa kampeni hiyo na kuachiliwa kwa mateka wote waliosalia.
Kwa mujibu wa shirika la mtandao wa BBC, waandamanaji wakipeperusha mabango na kushikilia picha za mateka hao ambao bado wanashikiliwa huko Gaza, wameitaka serikali ya Netanyahu kuingia kwenye majadiliano na wanamgambo wa Hamas, ili wapendwa wao waweze kuwa huru.
Idadi ya washiriki ilikadiriwa kuwa makumi kwa maelfu, wakati Jukwaa la Familia za Watekaji lilisema hadi watu 100,000 walishiriki katika maandamano hayo, kulingana na Agence France-Presse.
Shirika hilo pia limemnukuu Shahar Mor-Zehero, jamaa wa mateka waliouawa akisema, “Tutahitimisha kwa ujumbe wa moja kwa moja kwa Netanyahu: Ikiwa utavamia sehemu za Gaza na mateka wakauawa, tutawafuata katika viwanja vya miji, wakati wa kampeni za uchaguzi, na wakati wote na kila mahali.”
Ingawa mamlaka haijatoa makadirio rasmi ya idadi ya washiriki, inaonekana kuwa kubwa zaidi kuliko umati wa watu walioshiriki katika maandamano ya awali ya kupinga vita.
Ofisi ya waziri mkuu juzi Ijumaa ilitangaza kwamba Baraza la Mawaziri la Usalama, ambalo ni kundi dogo la mawaziri wakuu, limeamua kuuteka mji wa Gaza, na kupanua wigo wa operesheni za kijeshi katika eneo lililoharibiwa la Palestina, licha ya upinzani mkubwa wa umma na onyo la kijeshi kwamba hatua hiyo inaweza kuwahatarisha mateka.
Vita vya Gaza vilivyoanza baada ya mashambulizi ya Hamas ya tarehe 7 Oktoba 2023, vimesababisha mzozo mkubwa kufikia kiwango cha hatari kuliko wakati wowote katika historia ya mataifa hayo mawili.
Kuendelea kwa vita hivyo, kunaigawa Waisraeli, kunaua raia wengi zaidi wa Palestina na kunatia hofu mamilioni ya watu duniani, wakiwemo wanaojiita marafiki wa Israel.
Tayari mataifa kadhaa ulimwenguni, yamezidi kukasirishwa na ukatili unaofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Miongoni mwao, ni pamoja na Ufaransa, Uingereza na Canada, ambayo majuzi yametangaza mpango wa kulitambua taifa la Palestina, ikiwa ni sehemu ya kuchoshwa na vitendo vya Israel dhidi ya Wapalestina..
Mvutano ulikuwa umeongezeka hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza, lakini hekima iliyozoeleka ni kwamba si Hamas, kundi la Kiislamu linalotawala huko, wala Israel na badala yake, Hamas imekuwa ikipanga operesheni kali dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.
Hamas ina idadi kubwa ya roketi, kwa mfano ina kombora la masafa mafupi kama vile Qassam linaloweza kuruka umbali wa kilomita 10 na Quds 101 lenye uwezo wa kuruka kilomita 16, Grad linaloweza kuruka umbali wa kilomita 55.
Lakini Hamas lina roketi nyengine kama vile M-75 ambayo ina uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 75 na Fajr linaloweza kuruka umbali wa kilomita 100.
Aidha, Hamas wana roketi ya R-160 ambayo inaweza kuruka umbali wa kilomita 120 na M -302 ambayo inaweza kurushwa kwa umbali wa kilomita 200.
Ni wazi kwamba Hamas ina silaha ambazo zinaweza kushambulia mji wa Tel Aviv na Jerusalem na zinaweza kufika umbali wa pwani ya taifa hilo, eneo ambalo idadi kubwa ya Waisraeli huishi, mbali na majumba muhimu na ofisi za serikali.
ZINAZOFANANA
Watu 18 wafa kwa njaa Ukanda wa Gaza
Vita vya Gaza: Hamas waapa kufia kwenye ardhi yao
Maadhimisho ya Nne ya Lugha ya Kiswahili yapokewa kwa bashasha Harare, Zimbabwe