
WIZARA ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema, imerekodi vifo 18 “kutokana na njaa” katika muda wa saa 24 zilizopita. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa, Gaza … (endelea).
Siku ya Jumamosi wizara hiyo ilionya kwamba njaa kali inaongezeka huko Gaza na idadi ya watu wanaofika katika vituo vyake “wakiwa na uchovu mwingi inaongezeka.”
“Tunaonya kwamba mamia ya watu ambao miili yao imechoka wako katika hatari ya kifo kutokana na njaa,” imeleeza taarifa hiyo na kuongeza, “watu wanakufa” na hivyo, ni lazima Umoja wa Mataifa (UN), uingilie kati.
UN umekiri kuwa huko Gaza watu wanakufa njaa na kutoa wito wa kuingizwa kwa haraka bidhaa muhimu.
Nje ya hospitali Shifa katika mji wa Gaza mwanamke mmoja ameiambia BBC Arabic kwamba “Watoto wanakufa kwa njaa kwa sababu hawana chakula. Watu wanaishi kwa maji na chumvi… maji na chumvi tu,” alisema.
Shirika la UN la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika taarifa iliyotumwa kwenye X, ilisema kuwa “utapiamlo unaongezeka huku wanawake na watoto 90,000 wakihitaji matibabu ya haraka.”
Shirika hilo limesema, “Takriban mtu mmoja kati ya watatu hawali kwa siku.”
Haya yanatokea wakati vitisho vya vita vinazidi kuongezeka huko Gaza. Viungo vya watu waliofariki vikitapakaa mitaani na maelfu ya watu wanaokabiliwa na njaa, wakikodolewa macho na kifo.
Tayari Umoja wa Mataifa, umeonya kuwa maafa ya kibinadamu huko Gaza yanageuka kuwa njaa inayosababishwa na mwanadamu.
Imeitaka Israel kutekeleza majukumu yake ya kisheria ya kuwalinda raia wa Palestina, na kuruhusu usambazaji wa kutosha wa misaada ya kibinadamu kuwafikia watu wanaohitaji.
Kamishena Mkuu wa UN, anayeshughulikia haki za binadamu, Volker Türk, amesema katika taarifa yake kwamba Israel inalaumiwa kutumia njaa kama silaha ya vita vyake na Hamas.
Msururu mrefu wa malori yaliyosheheni vifaa vya msaada vinavyohitajika Ukanda wa Gaza yako upande wa Misri wa mpaka na Rafah, na kwamba yanaweza tu kuingia Gaza kupitia Israeli, baada ya ukaguzi tata na wa ukiritimba.
Kutokuwepo kwa vifaa vya kutosha kumeilazimisha Jordan, na sasa nchi nyingine ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, kurusha misaada kutoka angani – njia ya chini kabisa ya kusambaza misaada ya kibinadamu
ZINAZOFANANA
Vita vya Gaza: Hamas waapa kufia kwenye ardhi yao
Maadhimisho ya Nne ya Lugha ya Kiswahili yapokewa kwa bashasha Harare, Zimbabwe
Diogo Jota wa Liverpool afariki kwa ajalin