
MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25 umehitimishwa kwa mtanange mkali wa Kariakoo Derby uliopigwa Uwanja wa Mkapa, ambapo Yanga SC waliibuka kidedea kwa kuwalaza Simba SC mabao 2-0. Bao la kwanza lilifungwa na Pacome Zouzoua kupitia mkwaju wa penalti, kabla ya Clement Mzize kuongeza la pili katika dakika za mwisho.
Ushindi huo si tu uliwapa Yanga heshima mbele ya watani wao, bali pia uliwahakikishia ubingwa wao wa 31, wakiwa na pointi 82, nne zaidi ya Simba waliomaliza nafasi ya pili. Meridianbet walikuwa sambamba nawe mbashiri kwenye mizunguko yote ya ligi msimu huu kwa kukupa machaguo mengi kwenye michezo yote na odds kubwa Zaidi.
Katika msimu huu uliohusisha vilabu 16, kila timu ilicheza michezo 30 (nyumbani 15, ugenini 15). Timu nne zilizotamba juu ya msimamo ni Yanga, Simba, Azam na Singida Black Stars. Kutokana na nafasi zao, Yanga na Simba zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam na Singida wakielekea kwenye Kombe la Shirikisho.
NB: Jiunge na Meridianbet na ujionee ushindi rahisi kupitia michezo mbalimbali ya kasino ya mtandaoni. Pia unaweza kuongeza kipato chako kwa kubashiri mechi zenye ODDS KUBWA. Piga *149*10# au tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz
Kwa upande mwingine, Kagera Sugar na Ken Gold zimeshuka moja kwa moja kutoka Ligi Kuu, nafasi zao zikichukuliwa na Mtibwa Sugar pamoja na Mbeya City. Tanzania Prisons na Fountain Gate bado zina nafasi ya kubaki, lakini zitasubiri maamuzi ya mechi za mtoano dhidi ya Geita Gold na Stand United.
Msimu huu ulishuhudia upinzani mkali kwa upande wa wafungaji bora. Jean Ahoua wa Simba ndiye aliyemaliza kileleni na mabao 16, akifuatiwa kwa karibu na Clement Mzize wa Yanga aliyefunga 14. Hat-trick kadhaa zilirekodiwa, zikiwemo za Prince Dube (Mashujaa), Mukwala (Coastal Union), Stéphane Aziz Ki (KMC), pamoja na Ahoua (Pamba Jiji). Mchezaji aliyewasisimua wengi ni Sowah wa Singida BS, ambaye licha ya kusajiliwa dirisha dogo la usajili na kucheza nusu msimu, alifunga mabao 12 katika michezo 12 tu.
Kwenye lango, Mousa Camara wa Simba aliweka historia kwa kulinda clean sheet katika mechi 19, akiifikia rekodi ya Aishi Manula ya msimu wa 2017/18. Hata hivyo, matumaini ya kuivunja yakayeyuka baada ya Yanga kumpachika mabao mawili kwenye mechi ya mwisho ya msimu.
Zaidi ya matokeo, msimu huu ulileta mabadiliko ya kiutawala na kiufundi. Mara ya kwanza, mchezo wa Derby ulichezeshwa na waamuzi wa kigeni kutoka Misri, jambo lililosababisha mazungumzo mengi miongoni mwa wadau. Migomo kutoka klabu kubwa kama Simba na Yanga juu ya baadhi ya maamuzi ya bodi ya ligi ilisababisha mabadiliko katika safu ya uongozi wa juu.
Takwimu za safu ya mashambulizi kwa msimu huu ilishikiliwa na Yanga (mabao 83), Simba (69), huku Pamba Jiji, Ken Gold na Kagera Sugar zikiwa na safu dhaifu kwa kufunga mabao 22 kila mmoja. Kwa upande mwingine, safu za ulinzi pia zimeonyesha Yanga waliruhusu mabao 10 tu katika mechi zote 30, Simba wakafuata kwa mabao 13, na Azam waliruhusu 19. Kwa upande wa ulinzi hafifu, Ken Gold (62) na Fountain Gate (58) zilitikiswa mara nyingi zaidi.
Kama kawaida, mashabiki wa soka walifurahia msimu huu kupitia ubashiri wa michezo kupitia Meridianbet, waliotoa odds kubwa na ofa kabambe. Kama bado hujajiunga, huu ndio wakati wako. Jisajili sasa na uanze safari yako ya kubashiri michezo mingi zaidi na kujitengenezea kipato kwani ligi hazimaliziki huku.
ZINAZOFANANA
Juventus vs Man City kukupatia faida mara mbili leo
Benki ya NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu kwa Yanga
Yanga yaifikia rekodi ya Simba, yatwaa Ubingwa wa nne mfululizo