
Ratiba rasmi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa msimu wa 2025/26 imetangazwa leo, Juni 18 saa 9:00 asubuhi kwa saa za Uingereza, ikileta matumaini mapya kwa mashabiki wa soka duniani na hasa kwa wabashiri wa Meridianbet, kampuni inayoaminika zaidi kwa michezo ya kubashiri.
Msimu huu mpya utaanza rasmi Agosti 15, 2025 na utamalizika Mei 24, 2026, ukiwa na jumla ya mechi 380 zitakazochezwa katika raundi 38.
Mechi ya ufunguzi itakuwa Ijumaa, Agosti 15, ambapo mabingwa watetezi Liverpool watafungua msimu dhidi ya Bournemouth. Wikiendi hiyo itaendelea na raundi ya kwanza tarehe 16 na 17 Agosti, ikiwemo pambano la moto la Manchester United dhidi ya Arsenal, ambalo linatarajiwa kuvutia hisia kubwa kwa mashabiki na pia kuwa fursa ya pekee kwa wabashiri wa Meridianbet.
Katika mechi nyingine za raundi ya kwanza, Manchester City wataanza kampeni yao ugenini dhidi ya Wolves, huku Aston Villa wakiwakaribisha Newcastle pale Villa Park. Pia Brighton watacheza dhidi ya Fulham, Nottingham Forest dhidi ya Brentford, na Sunderland, waliopanda daraja, watakuwa wenyeji wa West Ham. Mabingwa wa Europa, Tottenham, watazindua msimu wao dhidi ya Burnley.
NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz
Miongoni mwa mechi zinazotarajiwa kwa hamu kubwa msimu huu ni pamoja na Derby ya Manchester itakayopigwa Septemba 13, pamoja na North London Derby kati ya Arsenal na Tottenham mwishoni mwa Novemba. Mechi hizi za hadhi ya juu huwa na mvuto mkubwa si tu kwa mashabiki bali pia kwa wabashiri, na kwa watumiaji wa Meridianbet ni fursa ya kukuza uchumi wao.
Raundi ya mwisho ya ligi itachezwa Mei 24, 2026, ambapo timu zote 20 zitashuka dimbani kwa wakati mmoja. Mara nyingi, siku hiyo huwa ni ya fainali kwa timu zinazopigania ubingwa, kuepuka kushuka daraja, au kufuzu michuano ya Ulaya, hivyo kuwa na mvuto wa pekee msimu huu.
Ratiba kamili ya mechi zote inapatikana kupitia tovuti rasmi ya EPL, ingawa tarehe na muda wa mechi zinaweza kubadilika kulingana na ratiba za matangazo ya moja kwa moja.
Kwa kuangalia maandalizi ya klabu mbalimbali, swali ni je, Liverpool wataweza kuutetea ubingwa wao? Arsenal na Manchester City watakuja kitofauti? Au pengine, msimu huu tutashuhudia yale ya msimu wa 2016 na timu isiyotegemewa kuibuka bingwa?
ZINAZOFANANA
Real Madrid vs Al Hilal kukupatia faida mara 2 leo
Sanlam Insurance kutumia Mbio za NBC Dodoma Marathon kufikisha elimu ya Bima
GSM kusambaza maji, vinywaji baridi kwa washiriki wa mbio za NBC Marathon