April 29, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kardinali Becciu ajiondoa kumchagua Papa mpya

Kardinali Giovani Angelo Becciu

 

KARDINALI Giovani Angelo Becciu wa Serdegna ametangaza kujitoa kushiriki kwenye mkutano wa uchaguzi wa Papa mpya unaotarajia  kufanyika tarehe 7 Mei 2025. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kardinali Giovani ametoa maamuzi hayo huku akisisitiza kutokuwa na hatia ila imempasa kutii utashi wa baba mtakatifu Francis kwa ajili ya maslahi ya kanisa.

Hatua hio ya kardinali Giovani imetokea wakati kanisa katoliki likijiandaa kwa mkutano wa kumchagua Papa mpya baada ya kifo cha papa Francis na nafasi kubaki wazi.

Baada ya kifo cha papa francis kanisa katoliki lipo kwenye maandalizi ya mchakato maalumu wa uchaguzi utakaofanyika katika kanisa la Sistine Vatican.

Kardinali Giovani amewahi kuwa mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa ndani ya Vatican akihudumu nafasi mbalimbali ikiwemo Naibu wa masuala ya ndani ya Vatican, na aliteuliwa na papa Francis.

Hata hivyo aliingia hatiani mwaka 2020 baada ya kuhusishwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za kanisa na zinginezo zilizopelekea Papa Francis kumwondoa katika wadhifa wake na kumpokonya haki ya kushiriki katika mikutano ya uchaguzi.

About The Author

error: Content is protected !!