April 29, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Amnesty yakosoa hatua za Trump akitimiza siku 100 madarakani

Rais wa Marekani, Donald Trump

 

SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International limetoa  ripoti yake ya kila mwaka na kukosoa vikali hatua za rais wa Marekani, Donald Trump ambaye ametimiza siku 100 akiwa madarakani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Amnesty imesema hatua za Trump zinalenga kurejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya umaskini duniani, kupambana na ubaguzi wa rangi na vipaumbele muhimu vya haki za binadamu.

Tangu alipoapishwa kuongoza muhula wa pili tarehe 20 Januari 2025, Trump amechukua hatua kadhaa ambazo zimeutikisa ulimwengu  kiuchumi, kijamii na kiusalama.

Baadhi, ni hatua za ushuru, kusitisha misaada ya kimataifa, sintofahamu na washirika wake wa NATO pamoja na vitisho vya kunyakuwa maeneo kama Gaza, Greenland, Mfereji wa Panama na kutaka kuifanya Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani.

About The Author

error: Content is protected !!