April 28, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mwanamke aishi hospitalini miaka 45 kwa kimakosa

Kasiba

 

MWANAMKE mmoja mwenye usonji na ulemavu wa kujifunza, ambaye ni raia wa Sierra Leone na alipewa jina la Kasiba na mamlaka za eneo kwa usalama wake, adaiwa kuzuiliwa kimakosa katika hospitali ya wagonjwa wa akili nchini Uingereza kwa miaka 45. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Idara ya Afya na Huduma za Jamii nchini Uingereza ilisema kuwa hali ya watu wengi wenye ulemavu kuhifadhiwa katika hospitali za akili ni hali isiyokubalika na kwamba mageuzi katika sheria za afya ya akili yatazuia mateso kama hayo.

Zaidi ya watu 2,000 wenye usonji na ulemavu wa kujifunza bado wako katika hospitali za akili nchini Uingereza.

Na baada ya ripoti ya mwanasaikolojia kumalizika ilionesha kuwa Kasiba hana ugonjwa wa akili, hana hatari yoyote na ana uwezo wa kuishi katika jamii.

Kasiba, ambaye sasa ana umri wa zaidi ya miaka 50, inadhaniwa kuwa aliletwa kinyume cha sheria kutoka Sierra Leone akiwa na umri wa miaka mitano.

Baada ya kuishi katika kituo cha watoto kwa muda, alihamishiwa hospitalini akiwa na umri wa miaka saba.

Huduma ya Afya ya Taifa (NHS) inakusudia kupunguza utegemezi wa vituo vya kuwahifadhi wenye magonjwa ya kiakili kwa watu wenye ulemavu wa kujifunza na usonji kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025-26.

About The Author

error: Content is protected !!