
MAHAKAMA ya juu ya Haki ya Umoja wa Mataifa hii leo imeanza kusikiliza madai kuhusiana na wajibu wa Israel katika kuhakikisha na kuwezesha uingizwaji wa msaada wa kibinadamu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Mahakama imeanza kusikiliza kesi hiyo kuangazia wajibu wa Israel katika kufikishwa kwa msaada wa kibinadamu unaohitajika haraka kwa raia wa Palestina walioko kwenye maeneo yanayokaliwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar, hata hivyo ameitaja kesi hiyo kama sehemu ya “ukandamizaji wa kimfumo na kuliharamisha” taifa lao.
Akizungumza mjini Jerusalem wakati kesi hiyo ikianza mjini The Hague, Saar amesema mahakama hiyo imekuwa ya kisiasa, na kuitaja kesi hiyo kuwa ni “aibu”.
Kesi hiyo itakayosikilizwa kwa wiki nzima, inafuatia ombi la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwaka jana, lililoiomba mahakama hiyo ya kimataifa hiyo kupima majukumu ya kisheria ya Israel baada ya kulizuia shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Palestina kufanya kazi kwenye eneo lake.
ZINAZOFANANA
Matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani kwa kiwango kikubwa
Makardinari kuchagua Papa mpya
Trump: Rais wa Ukraine ana nia ya makubaliano