Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama
TAMASHA la kuombea Uchaguzi Mkuu kufanyika mikoa 26 kuanzia jijini Dar es Salaam mwaka huu ambapo waimbaji mbalimbali wanatarajiwa kupamba tamasha hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Machi 24, 2025, Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema kuwa ibada hiyo itakuwa ni ya Maandalizi ya kuelekea Uchaguzi.
“Lengo ni kuweka umoja na ushirikiano watanzania kuombea uchaguzi kufanyika kwa Amani na kupata viongozi ambao watatuongoza kwa hekima na busara.
“Waimbaji kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda wanatarajia kupamba tamasha hilo la uimbaji na Maombi ya uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha ameongeza kwa kuwaomba viongozi wa vyama vya siasa kutumia lugha zisizo za matusi katika mikutano yao bali kutumia lugha za siasa zenye heshima hata kwa vizazi vyetu.
Pia amewaomba wadau na watu mbalimbali kujitokeza kutoa ushirikiano wa kudhamini ili kufanikisha tamasha hilo
ZINAZOFANANA
Ushindi upo nje nje siku ya leo na Meridianbet
Piga mkwanja na Meridianbet leo
Ijumaa ya kibingwa imefika ndani ya Meridianbet