February 19, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Meridiansports yarudisha kwa jamii

MABINGWA wa kuchapisha makala ya Michezo Mtandaoni Meridiansports wamefanikiwa kurudisha kwenye jamii kwa mara nyingine na leo wameifikia shule ya Sekondari ya Jangwani ya jijini Dar-es-salaam kuhakikisha inakua sehemu ya wanufaika wa msaada huo.

Huu umekua utartibu wa kampuni hii miaka na miaka kuhakikisha wanagawana kile kidogo wanachopata pamoja na jamii yao, Leo waliofanikiwa kufikiwa na mabingwa hao wa michezo ya kubashiri ni shule ya sekondari ya Jangwani.

Zoezi hili ni sehemu ya kampeni ya kusaidia afya na elimu kwa watoto wa kike kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata mahitaji muhimu ya kiafya yanayowawezesha kuhudhuria masomo yao bila vikwazo. Taulo za kike ni mahitaji muhimu kwa wasichana shuleni, na ukosefu wake unaweza kuwa changamoto kwa mahudhurio na maendeleo yao ya kitaaluma.

Kikawaida Meridiansports wamekua wakijitahidi kurudisha kwa jamii yake na hua wanarudisha pale ambapo kuna uhitaji mkubwa, Kama ambavyo shule ya Sekondari Jangwani imefikiwa kwakua imeonesha kukidhi vigezo na ni wazi wasichana wa shule hiyo walikua na uhitaji mkubwa wa mataulo ili kuweza kuimarisha mazingira yao ya kiafya.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Muhariri wa Meridiansports, Nancy Ingram, alisema, “Tunatambua umuhimu wa elimu kwa kila mtoto wa kike na changamoto wanazokumbana nazo wanapokosa vifaa muhimu vya usafi wa kibinafsi. Hii ndiyo sababu Meridiansports inajitahidi kusaidia jamii kwa kuhakikisha wasichana wanapata msaada wanaohitaji ili waweze kusoma bila changamoto.”

Meridiansports imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwa ni pamoja na elimu, afya, na mazingira. Kampuni hiyo inaendelea kutekeleza programu zake za uwajibikaji wa kijamii ili kuhakikisha jamii inafaidika kwa njia endelevu.

Aidha Mwakilishi kutoka shule ya Jangwani Sekondari, aliishukuru Meridianbet kwa msaada huu muhimu na kueleza kuwa, “Msaada huu utasaidia kupunguza changamoto wanazokutana nazo wanafunzi wetu wa kike. Tunawashukuru Meridiansports kwa kuona umuhimu wa kusaidia wasichana wa shule yetu.”

About The Author

error: Content is protected !!