
MKONGWE katika muziki nchini Uganda, Bebe Cool anazidi kuchanja mbuga na kibao chake ‘Circumference’ alichoachia hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Singo hiyo ambayo ameirekodi katika mfumo wa video, ni utayarisho wa ujio wa albamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Break The Chains’ atakayoachia mapema mwezi Aprili, mwaka huu.
Kazi hiyo iliyorekodiwa katika vivutio mbalimbali nchini Afrika Kusini imeongozwa na mwogozaji daraja la kwanza, Garrick Williams – itakupa raha ya kuufaidi uzuri wa mandhari za nchini Afrika Kusini.
Akizungumzia video yake hiyo na matayarisho ya ujio wa albamu yake mpya, Bebe Cool anasema: “Ujio wa wimbo wangu wa Circumference ni mwanzo wa ukurasa wangu mpya katika safari ya muziki.
“Ninafurahi kuwapa mashabiki na dunia nzima ladha hii nzuri ya muziki mzuri.”
ZINAZOFANANA
Afrika yazidi kuchanja mbuga mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026
Ofa kabambe ya karibu kwa wateja wapya wa Meridianbet.
Bashiri bingwa wa EPL na Meridianbet umalize msimu kitajiri