TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)- Bara, amesema kuwa amesema pamoja kutofautiana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kwa misimamo lakini hawajawahi kugombana. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu amesema hayo leo tarehe 21 Januari 2025 wakati akitoa salamu zake kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa chama hicho.
“Tunaweza kuwa tumetofautiana kimsimamo lakini hatujawahi kugombana”, amesema Lissu.
Lissu amesema kuwa uamuzi wowote utakaofanywa na wajumbe wa chama hicho ni sehemu ya ujenzi wa chama naye ni muumini wa ujenzi wa chama hicho. “vyovyote itakavyokuwa leo nitakuwa mmoja wa kujenga chama chetu.”
Leo wajumbe wa chama hicho watafanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa chama hicho, huku mchuano mkali ukiwa kwa Lissu na Mbowe lakini naye Odero Charles Odero akiwa hayupo nyuma kwenye mapambano hayo.
Pia wajumbe hao watamchagua Makamu Mwenyekiti Bara ambapo kuna mchuano mkali kati ya John Heche mjumbe wa zamani wa Kamati Kuu na Ezakia Wenje.
ZINAZOFANANA
Mbowe afungua Mkutano Mkuu akilia na matusi
Jumuiya ya Wazazi CCM yawapiga biti mavimba macho Urais CCM 2025
Mwabukusi: Chadema tutawaadhibu, msipowasiliza wananchi