TAKRIBAN watu 78 wamefariki dunia, baada ya boti kupinduka katika Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana.
Taarifa zinaeleza kuwa zaidi ya watu 100 waliokuwa wamepanda boti hiyo hawajulikani walipo.
Gavana wa Jimbo la Kivu Kusini, Jean Jacques Purisi, amethibitisha taarifa hizo, na kuongeza kuwa watu 278 walikuwa wamepanda boti hiyo, kabla ya kupinduka.
“Itachukua angalau siku tatu kupata namba kamili, kwa sababu sio miili yote imepatikana,” Purisi ameiambia Reuters.
Hata hivyo, Gavana wa jimbo jirani la Kivu Kaskazini, amesema takriban watu 58 wameokolewa.
Maofisa wa uokoaji wanaendelea na juhudi za kutafuta manusura, huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.
Kwa habari zaidi.
ZINAZOFANANA
Samia kutikisa Brazil mkutano wa wakuu wa kundi la G20
Waziri Kijaji afanya mazungumzo na wadau wa COP29
Korea Kusini lawamani kukandamiza uhuru wa dini