September 18, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Barcelona, Liverpool na Man City wamewakaa

 

Wakati huu msimu mpya wa ligi mbalimbali duniani ukiwa umerejea barani ulaya vilabu kadhaa vimeonekana kuuanza msimu vizuri na kuonesha mwanga mzuri mapema huenda wakafanya vizuri msimu huu.

Pale kwenye ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City ambayo ndio bingwa mtetezi ameonekana kuanzia pale alipoishia msimu uliomalizika kwani mpaka sasa wameshafanikiwa kushinda michezo yao mitatu ya awali, Liverpool wao chini ya kocha mpya Arne Slott nao wameanza msimu vizuri ambapo wameshinda michezo yao mitatu ya awali hii ikionesha ishara nzuri kwa upande wao.

Ligi kuu ya Hispania Barcelona wao wamekuja kitofauti chini ya kocha Hans Flick kwani wameonekana kucheza mpira mzuri lakini pia wanatoa dozi kubwa kwa wapinzani, Mpaka sasa wameshinda michezo yao yote mitatu ya mwanzo huku wakifunga mabao mengi, Wapinzani wao Real Madrid hali imekua tofauti kwani wametoa sare michezo miwili kati mitatu.

Kunako ligi kuu ya soka nchini Ufaransa PSG mabingwa watetezi nao wameonekana kuanza kwa kasi na kuhitaji kutetea taji lao kikamilifu, Kwani kwenye michezo mitatu ya awali wameshinda michezo yote, Huku klabu ya Olympique Marseille wakiwafata kwa ambao wameshinda michezo yao miwili kati ya mitatu na kusare mchezo mmoja.

Ligi kuu ya soka nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga haijaanza vizuri kwa mabingwa watetezi wa Bayer Leverkusen ambao walimaliza msimu bila kupoteza mchezo wowote, Lakini msimu huu tayari wameshapoteza mchezo mmoja kati ya miwili waliyocheza huku wapinzani wao Bayern Munich wakishinda michezo yao yote miwili.

Seria A ligi kuu ya soka nchini Italia nayo imeanza kurindima ambapo mabingwa watetezi klabu ya Inter Milan imeanza vizuri msimu kwani inaongoza msimamo wa ligi hiyo mpaka sasa wakiwa na alama 7 kwenye michezo mitatu wakifungana na Juventus ambao nao wameanza msimu vizuri.

Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko sehemu yeyote ile, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.

About The Author