September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Meli yazama ikiwa na abiria 300, miili 20 yaopolewa

ZAIDI ya watu 300 wanahofiwa kufa maji katika ajali ya meli iliyotokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili tarehe 18 Agosti kwenye Mto Lukenie. Ajali hiyo imetoke katika eneo la Kutu, mkoa wa Mai-Ndombe, kusini-magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Meli hiyo iliyokuwa ikielekea Nioki ikiwa imebeba zaidi watu 300 na bidhaa mbalimbali ilizama na hadi sasa ni takriban miili 20 pekee ndiyo imepatikana.

Meli hiyo iliondoka katika mji wa Amo kwenye ukingo wa Mto Kongo, zaidi ya kilomita 600 mashariki mwa Kinshasa.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mbali na abiria waliokuwemo, ilikuwa imebeba chakula.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa wilaya ya Kutu nchini humo, Jacques Nzenza amesema meli hiyo ilianza safari muda wa jioni ambao ulipigwa marufu kwa kwa safari za meli lakini nahodha wa meli hiyo aliendelea na safari kuelekea Tolo.

“Alipofika mahali paitwapo Maurice, ni sehemu ya wavuvi, meli hiyo ilitaka kupinduka na iliposogea mbele kidogo iligonga vipande vya mbao vilivyokuwa kando na pinduka,” amesema

Amesema Jumanne jioni, miili mingine 16 iliopolewa pamoja na minne iliyopatikana siku ya Jumapili.
“Mara nyingi wamiliki wa meli wanatoa rushwa na kushirikiana na mamlaka ya bandari na idara za usalama kuruhusu safari hizo za usiku. Wanafanya chochote wanachoweza,” ameongeza mkuu wa wilaya ya Kutu.

About The Author