Siasa

Siasa

Wabunge 5 CUF wabanwa mbavu Handeni

WABUNGE watano kutoka Chama cha Wananchi (CUF), tarehe 3 Agosti 2019 walikamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi wilayani Handeni, Tanga kwa madai ya kufanya mkutano bila kibali. Anaandika Danson ...

Read More »

Rais Magufuli awapa zawadi wafungwa

RAIS John Magufuli leo tarehe 16 Julai 2019, ametoa zawadi ya magunia 15 ya mchele pamoja na ng’ombe watatu kwa wafungwa na mahabusu waliopo kwenye gereza kuu la Butimba, jijini ...

Read More »

Sakata la Lissu: Wabunge CCM wamlalamika Ndugai

BAADHI ya wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameeleza kutofurahishwa na kitendo cha Job Ndugai, Spika wa Bunge kumvua ubunge Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). Wakizungumza kwa sharti la kutoandikwa majina ...

Read More »

Kesi ya Mbowe, wenzake:Shahidi aibua mapya

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeendelea kusikiliza kesi namba 112 ya mwaka 2018 ya viongozi wa Chadema leo tarehe 1 Julai 2019.Anaripoti Faki Sosi …(endelea). Shahidi wa tano wa Jamhuri, daktari ...

Read More »

Kodi taulo za kike: Zitto ajenga hoja

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amepinga pendekezo la serikali la kurejesha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kwenye taulo za kike. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea). Mwanasiasa huyo mashuhuri leo ...

Read More »

Lipumba maji ya shingo, Maalim Seif kicheko

KWA mara ya kwanza, Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amekiri kwamba, chama chake kinahemea pomoni. Anaandika Mwandishi Wetu …(endelea). Tofauti na awali ambapo, Prof. Lipumba na ...

Read More »

Prof. Safari: AG anaweza kutenda jinai

MBOBEZI wa sheria nchini na Wakili wa Mahakama Kuu, Prof. Abdallah Safari amesema, iwapoDk. Adelardus Kilangi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), atagoma kutekeleza hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar ...

Read More »

Prof. Lipumba amtumia Lowassa kujiimarisha

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ameanza kumtumia Edward Lowassa aliyerejea CCM kujiimarisha kisiasa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea). Kiongozi ...

Read More »

CCM, UKAWA watafunana Muswada wa Vyama vya Siasa

WABUNGE kutoka chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale kutoka vyama vya upinzani wameanza kumenyana kuhusu Muswada mpya wa Vyama vya Siasa uliowasilishwa bungeni leo tarehe 29 Januari 2019. Anaripoti ...

Read More »

Wapinzani wajibu mashambulizi Muswada Vyama vya Siasa

MUSWADA wa Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya siasa umetua bungeni leo huku Kambi Rasmi ya Upinzani ikianisha hoja zake kupinga muswada huo. Anaripoti Tibason Kaijage…(endelea) Akiwasilisha bungeni leo tarehe 29 ...

Read More »

Mabilioni yaibwa kwa Jaji Mutungi

MAMILIONI ya shilingi ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yaliyotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake ndani ya vyama vya siasa nchini, hayajulikani yalipo, anaandika Shabani Matutu. ...

Read More »

Mpina wanaponda watia nia wenzake

MBUNGE wa Kisesa, Luhanga Mpina (CCM), amewaponda baadhi ya watangaza nia wenzake ambao hawakuhudhuria wakati wa uwasilishwaji wa Bajeti kuu ya mwaka wa fedha 2015/16. Anaandika Dany Tibason, Dodoma…(endelea). Amesema ...

Read More »

Serikali isipojiheshimu na ikachokwa, alaumiwe nani?

KUNA barua ya Josephat Butiku, ambaye wengi tunafahamu kama mwana CCM halisi na ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation (MNF), aliyomwandikia Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambayo Fred Mpendazoe ameinukuu ...

Read More »

Edward Moringe Sokoine: Jabali la kisiasa lisilosahaulika

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akiwa na marehemu Edward Moringe Sokoine

MIAKA 31 iliyopita, taifa hili lilipoteza mmoja wa viongozi mahiri, shupavu, na kipenzi cha wanyonge, Edward Moringe Sokoine. Kifo chake kilikuwa pigo kubwa kwa kuwa alikuwa tayari amejitokeza na kujipambanua ...

Read More »

Nchi imelazimisha vijana kukosa ajira

Baadhi ya vijana waliojitokeza kwenye usaili wa ajira za Uhamiaji

LINAPOKUJA suala la ajira kwa vijana wazungumzaji wakubwa sio vijana wasio na ajira, bali wale waliofanikiwa au viongozi wa kiserikali ndiyo huzungumza na kujaribu kujibu maswali ya kwa nini vijana ...

Read More »

CCM yadhihirisha ZAN-ID mtaji

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimethibitisha kunufaika na utaratibu wa kuhusisha haki ya kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi na maslahi ya kisiasa baada ya wawakilishi wake wote kushikamana na kuikataa hoja binafsi ...

Read More »

Wafugaji waigaragaza KADCO

KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ameonja joto ya jiwe. Wiki mbili zilizopita, alipokelewa kwa maandamano makubwa na halaiki na wananchi wa kabila la Maasai kutoka vijiji ...

Read More »

Serikali ingepanua kwanza magereza

MKUTANO wa 19 wa Bunge la Jamhuri umemalizika mkoani Dodoma. Pamoja na mengine, umepitisha “Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni.” Katika Bunge ...

Read More »

Makonda hana usafi wa kumtuhumu Gwajima

ANAYEITWA mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ameelekeza asichokiamini na; anataka kutenda asichokuwa na mamlaka ya kukitekeleza. Anaandika Saed Kubenea … (endelea). Amesema amemuita ofisi kwake Askofu wa Kanisa ...

Read More »

Kwa sababu hizi, CCM wamekosa kura yangu

ZAIDI ya miaka 50 sasa, Tanzania imekua chini ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tumekuwa katika mfumo wa chama kimoja hadi mwaka 1992, Watanzania waliporidhia demokrasia ya vyama vingi. ...

Read More »

Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu muswada wa Mahakama ya kadhi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSIANA NA MUSWADA WA MAHAKAMA YA KADHI Sisi, Maaskofu kutoka TEC, CCT na CPCT tumekutana leo tarehe Machi 30, ...

Read More »

Zitto Kabwe: Historia haiheshimu wanaojikweza

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hatimaye kimetua mzigo uliokielemea kwa muda mrefu. Ni kuondoka kwa Zitto Zuberi Kabwe katika chama hicho. Zitto, aliyepata kuwa naibu katibu mkuu, mbunge wa ...

Read More »

Zitto anajua makosa yake Chadema

UPO msemo uliotoholewa kutoka kwenye lugha ya Kiingereza –“Ukishindwa kupigana nao, ungana nao”. Kwa kutumia maneno mengine mepesi unaweza kusema, jifunze kukubaliana na matokeo. Kwamba asiyekubali kushindwa siyo mshindani. Inavyoonesha, ...

Read More »

Prof. Baregu: Zitto ni mzigo

PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye. Anandika Saed Kubenea ...

Read More »

Bora Pinda akose urais nchi ibaki salama

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ameshiriki kikamilifu kubomoa misingi ya taifa hili. Ni kutokana na kutaka kuwapo Mahakama ya Kadhi nchini. Anaandika Eberi M. Manya … (endelea). Ameahidi ndani ya Bunge Maalum ...

Read More »

Zitto: ACT kinaendana na kile nilichokipigania

BAADA ya minong’ono ya muda mrefu hatimaye, Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo. Zitto aling’atuka Ubunge, Alhamisi ...

Read More »

Askofu Kilani amkana Kardinali Pengo

ASKOFU Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini, amekana kujiengua na viongozi wenzake wa madhehebu ya Kikristo wanaosisitiza waumini wao kupigia kura ya hapana Katiba Pendekezwa.  Anaandika Saed Kubenea … ...

Read More »

Propaganda hadi mauaji?

PHILIP Mangula- Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, naye amejitumbukiza katika tope la njama za mauaji. Anaandika Christian Mwesiga … (endelea). Ametajwa na Khalid Kangezi, kuwa ni miongoni ...

Read More »

Kardinali Pengo umekosea, wengi wape

NANAMSHUKURU Mungu kwa kuniamsha salama, mwenye afya njema na akili timamu. Mnamo tarehe 10 Machi 2015, Jukwaa la Wakristo nchini lilitoa tamko kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufikia kuwahamasisha waumini wa ...

Read More »

Mchungaji Mtikila aiokoa CCM

MWENYEKITI wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amekisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujinasua na kitanzi cha waamini wa madhehebu ya Kiislamu wanaotaka kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini, ili ...

Read More »

Jerry Silaa awakacha waandishi

MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, amewakimbia waandishi wa habari aliowaita kuzungumza nao ofisini kwake, Ilala, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Sarafina Lidwino … (endelea). Silaa ambaye ni diwani ...

Read More »

Chadema yambwaga Zitto mahakamani

SAFARI ya mapambano kati ya Zitto Kabwe-Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imefika ukiongoni baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutupilia ...

Read More »

Kapteni Komba azidi kumliza Lowassa

WIKI moja tangu Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba (CCM) afariki dunia, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ameendelea kumlilia akimtaja kama mmoja wa makamanda wa kuongoza harakati za kumshawishi ...

Read More »

Bosi TCAA ajikoroga utetezi wa fedha za Escrow

MKURUGENZI wa Idara ya Udhibiti masuala ya Kiuchumi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dk. James Diu, amekiri kupokea kiasi cha sh. milioni 80.8 kutoka kwa James Rugemalira, lakini “akajikoroga” kuhusu ...

Read More »

Chadema yatwaa Mji mdogo Katoro

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimechaguliwa kuuongoza Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita, baada ya kukibwaga Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaandika Mwandishi wetu…(endelea). Mkurugenzi wa Halmashauli ya Wilaya ya ...

Read More »

Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania

BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA  BARUA YA KICHUNGAJI “Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu” (Lk. 21: 19) Sisi Maaskofu wenu tulikutana kusali na kutafakari pamoja huko Arusha tarehe 16 ...

Read More »

Ratiba ya uandikishaji wa wapiga kura mkoa wa Njombe

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIATUME YA TAIFA YA UCHAGUZI             UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA MKOANI NJOMBE Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia ...

Read More »

Mkakati wa kumuua Dk. Slaa wavuja

Mabere Marando na Benson Kigaira

MABERE Marando- Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Madendeleo (Chadema), amefichua mawasiliano ya siri yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya chama, na mkakati wa kumdhuru Katibu ...

Read More »

NIDA: Mradi wa kunufaisha wakubwa

DICKSON Mwaimu, mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ameliibua upya sakata la mradi wa vitambulisho vya taifa. Anaandika Saed Kubenea…(endelea).aifa (NIDA0, Dickson Maumi Amenukuliwa akisema, uandikishaji mpya mikoani haufanyiki ...

Read More »

Rais Kikwete atawaachia nini albino?

RAIS Jakaya Kikwete, aliyebakiza miezi saba tu ya kustaafu uongozi, yupo kwenye mtihani mgumu wa kutakiwa kufanya uamuzi kabla hajaachia madaraka. Anaandika Jabir Idrissa… (endelea). Katika muda huo, ana uchaguzi ...

Read More »

RC Ruvuma ameshindwa kuwajibisha wezi Mbinga

GAZETI la Nipashe Jumapili tarehe 27 Julai mwaka jana, lilibeba ujumbe mzito, ulioandikwa na Gideon Mwakanosya, kutoka Songea mkoani Ruvuma, kwamba “Mkuu wa mkoa wa Ruvuma (RC), ameahidi kuwashughulikia watakaohujumu ...

Read More »

Huyu ndiye Rais Pohamba mshindi wa tuzo ya Mo Ibrahim

RAIS anayeondoka madarakani nchini Namibia, Hifikepunye Pohamba (79), ameingia kwenye historia ya washindi wa tuzo ya dola milioni tano ya Mo Ibrahimu ya uongozi wa Afrika. Rais huyo ambaye anatarajiwa ...

Read More »

Zitto aomba achunguzwe

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, ameombwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), zichunguzwe. Anaandika Mwandishi wetu…(endelea). “Naiomba Sekretariati ...

Read More »

CCM washtakiana kwa Kinana

JOTO la uchaguzi mkuu linazidi kupanda ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na sasa makada wake wameanza kushitakiana wakituhumiana kuanza kampeni kabla ya wakati. Anaandika Edson Kamukara…(endelea). Mbunge wa Tabora ...

Read More »

Kilwa watakiwa kuitosa CCM

WANANCHI wa mikoa ya Kusini wametakiwa kutobweteka kwa mafanikio madogo ya ujenzi wa barabara badala yake, wametakiwa kukiondoa Chama Cha Mapinduzi madarakani kwa kuichagua Chadema. Anaandika Mwandishi wetu…(endelea). Akizungumza na ...

Read More »

Wanawake CUF wambana Shaka

KATIBU wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, emetakiwa kuwa makini katika matamko yake ili kujiepusha na uongo. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea). Onyo hilo kali limetolewa ...

Read More »

Mbowe: Serikali iwajibike mauaji ya albino

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman, ameitaka Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwasaka na kuwakamata wauaji wa walemavu wa ngozi (albino) na vikongwe. Anaandika Mwandishi wetu…(endelea). ...

Read More »

Kikwete, Lungu hawajui Tazara iko mahututi

RAIS Jakaya Kikwete na mwenzake wa Jamhuri ya Zambia, Edgar Lungu, wameahidi kushirikiana ili kuimarisha reli inayounganisha nchi hizi mbili (Tazara), ili kukuza biashara na uwekezaji. Akizungumza na waandishi wa ...

Read More »

Asasi za kiraia zaachwa “njia ya panda”

UTOAJI wa elimu kwa mpiga kura kuhusu Katiba Mpya upo “njia panda”. Mpaka sasa haijulikani ni lini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Asasi za Kiraia zitatoa elimu hiyo ...

Read More »

CCM yaanza kuporomoka

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimejiandikia historia yake mpya ya kisiasa. Kimeangusha kwa kishindo Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi wa marudio wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ...

Read More »
error: Content is protected !!