RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema Lebanon si sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki mbili yaliyoafikiwa, akiliita suala la Lebanon kuwa mzozo tofauti. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Kauli ya Trump imekuja huku Israel ikifanya wimbi kubwa la mashambulizi dhidi ya Lebanon baada ya makubaliano hayo kutangazwa.
Iran kwa upande wake imesema itakomesha usitishaji mapigano kwa upande mmoja ikiwa mashambulizi ya Israel yataendelea dhidi ya Lebanon.
Wizara ya Afya ya Lebanon imetangaza idadi ya vifo kutokana na mashambulizi makubwa ya Israel jana kuwa watu 182.
Kundi la Hezbollah limesema hivi leo limevurumisha maroketi kuelekea Kaskazini mwa Israel kujibu mashambulizi hayo.
ZINAZOFANANA
Guterres apongeza sitisho la vita
Hongereni Wananchi mmeilinda Iran-Mojtaba Khamenei
Trump ajigamba kushinda vita dhidi ya Iran baada ya makubaliano