Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amekaribisha tangazo la kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili kati ya Marekani na Iran. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Kupitia msemaji wake, Guterres ametoa wito kwa pande zote kuheshimu sheria za kimataifa na masharti ya makubaliano hayo, akisisitiza kuwa sitisho hilo ni muhimu kulinda maisha ya raia na kupunguza mateso ya kibinadamu yanayosababishwa na vita.
Aidha, Guterres alithamini juhudi za upatanishi zilizofanywa na nchi mbalimbali, ikiwemo Pakistan, katika kufanikisha makubaliano hayo.
Ujumbe huo unakuja huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kufanikisha makubaliano ya kudumu yatakayorejesha utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati.
ZINAZOFANANA
Hongereni Wananchi mmeilinda Iran-Mojtaba Khamenei
Trump ajigamba kushinda vita dhidi ya Iran baada ya makubaliano
Museveni na Kikwete wakutana kujadili Amani ya Sudani Kusini