April 8, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Trump ajigamba kushinda vita dhidi ya Iran baada ya makubaliano

Spread the love

RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema hana shaka kuwa taifa lake limepata ushindi kamili kufuatia makubaliano ya kusitisha vita kwa muda wa wiki mbili kati yake na Iran. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Akizungumza leo Jumatano 8 Aprili 2026 katika mahojiano na Shirika la Habari la AFP baada ya kutangaza hatua hiyo, Trump amesema suala la urani iliyorutubishwa na Iran litajadiliwa kwa kina chini ya makubaliano hayo.

“Vinginevyo nisingekubali,” amesema Trump bila kufafanua kwa kina hatua ambazo zingechukuliwa iwapo masharti hayo yasingefanikiwa.

Alipoulizwa kama angeweza kurejea kutoa vitisho kama vya awali vya kushambulia miundombinu muhimu ya Iran, ikiwemo mitambo ya nishati na madaraja, Trump amejibu kwa kifupi: “Utalazimika kufuatilia hili.”

Trump anatarajiwa kusafiri kwenda China mwezi ujao kwa mazungumzo na kiongozi wa nchi hiyo, Xi Jinping katika ziara inayotazamiwa kuangazia pia masuala ya usalama wa kimataifa na ushirikiano wa kiuchumi.

About The Author

error: Content is protected !!