RAIS wa Marekani Donald Trump ametoa tishio jipya kwa Iran akionya kwamba mashambulizi makubwa yanaweza kutokea leo usiku huku muda wa mwisho aliotoa kwa Iran kufanya makubaliano na kufungua Mlango-Bahari wa Hormuz ukikaribia. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Trump amechapisha kwenye mtandao wa Truth akionya mfumo mzima utaangamizwa leo na hautarejeshwa tena.
“Tutabaini usiku wa leo,moja ya nyakati muhimu zaidi katika historia ndefu na ngumu ya dunia,miaka 47 ya dhuluma,ufisadi na vifo hatimaye itafikia mwisho.Mungu awabariki watu wa Iran”Alisema Donald Trump
Tishio hilo linakuja siku moja baada ya Trump kusema kwamba Marekani itaharibu kila daraja na kituo cha nishati nchini Iran ikiwa makubaliano hayatafikiwa .
ZINAZOFANANA
Rais wa Sudan kusin,amtimua Spika na Naibu Spika
Gavana wa zamani Urusi ahukumiwa miaka 14 Gerezani kwa Rushwa
Marekani kutoza tozo meli Hormuz