MAHAKAMA ya Urusi imemuhukumu Gavana wa zamani wa eneo la Kursk, Alexei Smirnov, kifungo cha miaka 14 jela kwa ufisadi. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es salaam …(endelea).
Msururu wa maafisa wa zamani katika mkoa wa Kursk, eneo la mpaka ambalo sehemu zake zilikamatwa na Ukraine kwa miezi kadhaa mnamo 2024, wamefunguliwa mashitaka kama sehemu ya uchunguzi wa ubadhirifu wa pesa zilizokusudiwa kwa ulinzi wa mipaka.
Smirnov, ambaye alishikilia wadhifa huo kuanzia Mei hadi Desemba 2024, alikabiliwa na tuhuma za kupora fedha za serikali, uhalifu aliofanya pamoja na maafisa wengine na wakandarasi waliopewa jukumu la kujenga miundo ya ulinzi.
Amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela pamoja na faini ya Dola Milioni 5. Pia amepigwa marufuku kushikilia wadhifa wa umma kwa muongo mmoja baada ya kuachiliwa kwake.
Mamlaka ya Urusi pia iliamuru kwamba Dola 261,300 ambazo alikiri kupokea kama hongo, zichukuliwe.
ZINAZOFANANA
Marekani kutoza tozo meli Hormuz
Milio ya risasi yasikika karibu na Ikulu ya Marekani, uchunguzi waanza
Rais Tshisekedi awatunuku nyumba na gari kila mchezaji kwa kufuzu kombe la Dunia