April 7, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Marekani kutoza tozo meli Hormuz

Spread the love

RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema nchi yake inaweza kuanzisha mfumo wa kutoza ada kwa meli zinazopita katika Mlango wa Hormuz baada ya vita kumalizika, akidai kuwa Marekani ndiyo mshindi wa mapambano hayo. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Kauli hiyo imekuja wakati mvutano ukiendelea Mashariki ya Kati, ambapo njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani imeathiriwa na vita vinavyoendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari, Trump amependekeza kuwa badala ya Iran kutoza ada kwa meli, Marekani inaweza kufanya hivyo yenyewe, akisisitiza kuwa ina haki hiyo kutokana na ushindi wa kijeshi.

“Kwa nini sisi tusitoze? Sisi ndio washindi,” amenukuliwa Trump.

Mlango wa Hormuz ni njia muhimu inayounganisha Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Hindi, na hupitisha takribani asilimia 20 ya mafuta ya dunia.

About The Author

error: Content is protected !!