April 8, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Hongereni Wananchi mmeilinda Iran-Mojtaba Khamenei

Mojtaba Khamenei

Spread the love

KIONGOZI Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei, ametoa pongezi kwa Wananchi wa Iran kufuatia kusitishwa kwa muda wa wiki mbili kwa vita kati ya Iran dhidi ya Israel na Marekani iliyoanza tangu 28 Februari 2026. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Khamenei ameelekeza pongezi zake kwa Wananchi wa Iran akisisitiza kuwa wao ndio waliobeba jukumu kubwa la kuilinda Nchi na kuwa mshikamano na uthabiti wao ndiyo vimeifanya Iran kuendelea kusimama imara katika kipindi chote cha mapigano “hongera kwa ushindi huu kwa Taifa la Iran na wapenda uhuru wote Duniani, ni ninyi Wananchi mlioiongoza Nchi”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vyombo vya Habari vya Iran, makubaliano ya kusitisha vita yanatarajiwa kujadiliwa Mjini Islamabaad Nchini Pakistan kuanzia 10 April 2026 ambapo Iran imeipa Marekani masharti kumi kabla ya kusitisha vita.

About The Author

error: Content is protected !!