April 7, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Gavana wa zamani Urusi ahukumiwa miaka 14 Gerezani kwa Rushwa

Spread the love

MAHAKAMA ya Urusi imemuhukumu Gavana wa zamani wa eneo la Kursk, Alexei Smirnov, kifungo cha miaka 14 jela kwa ufisadi. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es salaam …(endelea).

Msururu wa maafisa wa zamani katika mkoa wa Kursk, eneo la mpaka ambalo sehemu zake zilikamatwa na Ukraine kwa miezi kadhaa mnamo 2024, wamefunguliwa mashitaka kama sehemu ya uchunguzi wa ubadhirifu wa pesa zilizokusudiwa kwa ulinzi wa mipaka.

Smirnov, ambaye alishikilia wadhifa huo kuanzia Mei hadi Desemba 2024, alikabiliwa na tuhuma za kupora fedha za serikali, uhalifu aliofanya pamoja na maafisa wengine na wakandarasi waliopewa jukumu la kujenga miundo ya ulinzi.

Amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela pamoja na faini ya Dola Milioni 5. Pia amepigwa marufuku kushikilia wadhifa wa umma kwa muongo mmoja baada ya kuachiliwa kwake.

Mamlaka ya Urusi pia iliamuru kwamba Dola 261,300 ambazo alikiri kupokea kama hongo, zichukuliwe.

About The Author

error: Content is protected !!