Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa ‘Zungu la unga’ El Chapo kitanzini Marekani
Kimataifa

‘Zungu la unga’ El Chapo kitanzini Marekani

Joaquin Guzman ‘El Chapo’ muuza dawa za kulevya mkubwa katika bara la America akiwa chini ya ulinzi
Spread the love

UAMUZI wa Mexico kumpeleka nchini Marekani Joaquin Guzman ‘El Chapo’ muuza dawa za kulevya mkubwa katika bara la America unaonekana kulenga kummaliza kabisa mtukutu huyo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Mataifa ya Amerika yamekuwa kwenye vita dhidi ya biashara hiyo haramu iliyoshamiri huku ikiendeshwa na mitandao hatari ya matajiri.

Kumnasa El Chapo na hatimaye kumsafirisha nchini Marekani kumeongeza matumaini katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika bara la America kwani El Chapo alikuwa kiongozi wa genge maarufu la Sinaloa nchini Mexico.

Genge la El Chapo lilikuwa likiuza dawa za kulevya nchini Mexico na katika mataifa jirani ikiwemo Marekani, Argentina na Brazil jambo lililosababisha Marekani kumsaka kumtangaza kama mtu hatari anayesakwa kwa udi na uvumba.

Marekani ilikuwa ikimuwinda mfanyabiashara huyo hususan baada ya kutoroka gerezani mara mbili nchini Mexico akitumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kuchimba handaki liloingia gerezani na kumtorosha. Njama iliyosukwa na wasaidizi wake.

El Chapo pia alitoroka kupitia bomba lenye urefu wa kilometa 1.5 kupitia gerezani huku njama za kumtorosha zikidaiwa kusukwa na vigogo wa gereza kwa lengo la kumnusuru asipelekwe nchini Marekani.

Kabla ya kupelekwa Marekani wiki hii, mfanyabiashara huyo alikata rufaa mara kadhaa akipinga kupelekwa ugenini lakini hoja zake zikapuuzw na sasa yupo mikononi mwa Marekani na huenda ikawa ndiyo mwisho wa matukio yake ya kutoroka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

KimataifaTangulizi

Boti yazama DRC, 80 wafariki dunia

Spread the loveJUMLA ya watu 80 wameripotiwa kufariki dunia huko nchini Congo...

error: Content is protected !!