July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zumba na Kalulu kumwinda Mashali

Bondia Zumbe Kukwe

Spread the love

MABONDIA Zumba Kukwe ‘Chenji dola’ na Sweet Kalulu wanatarajia kupanda ulingoni Novemba 27 katika mpambano usiokuwa na ubingwa na mshindi atavaana na Thomas Mashali ayu Dullah Mbabe.

Mpambano huo ambao utakuwa wa raundi nne na usiokuwa na ubingwa, unatarajiwa kupigwa kwenye ukumbi Kontena, Kibaha, sambamba na mapambano mengine ya utangulizi.

Akizungumzia pambano hilo, mdhamini wa mpambano huo, George Nyasulu alisema wameamua mchezo huo upigwe Kibaha Maili Moja, alipotokea Zumba kwa lengo la kutanua wigo wa masumbwi nchini.

“Ngumi ziwe zinachezwa kila kona ya nchi, sio kila siku mabondia wanacheza jijini Dar es Salaam pekee. Watu wa mkoani nao pia wanahitaji kuona mchezo wa ngumi na kwa kuanzia tumeanza mkoa wa Pwani na tutaenda mikoa mingine kwa lengo la kuhamasisha,” alisema Nyasulu.

Mapambano ya utangulizi yatakuwa kati ya Mustafa Doto na Ramadhan Max, Shadrack Ignas na Fredy Masinde na Dogo Janja, na Issa Omar na Rajabu Miafro.

error: Content is protected !!