Spread the love

RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameshindwa kutokea kwenye kesi yake iliyounguruma leo katika Mahakama ya Pietermaritzburg katika jimbo la KwaZulu-nchini humo huku sababu ikitajwa kuwa anaumwa.

Aidha, wakati kesi hiyo ikirejewa leo tarehe 11 Aprili, 2022 barabara kadhaa zimefungwa karibu na mahakama hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa Mfuko wa Zuma, Mzwanele Manyi amesema tangu jana kigogo huyo hakuwa sawa kiafya.

“Tulidhani akiamka leo angeweza kuwa sawa kiafya na kuhudhuria hapa lakini hali yake bado haijatengamaa, hivyo madaktari walimshauri apumzike,” amesema.

Zuma anakabiliwa na kesi ya rushwa, utakatishaji fedha na ufisadi katika mkataba wa manunuzi ya silaha za kivita uliofanyika miaka 1990 wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani bilioni mbili.

Julai mwaka jana, maandamano ya ghasia yalizuka katika baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini baada ya Zuma kukamatwa na kutiwa gerezani kwa kosa la kuidharau mahakama.

Hata hivyo, mawakili wa Serikali wamelalamikia kitendo cha Zuma kushindwa kuhudhuria katika kesi hiyo na kudai kuwa anatumia mbinu hiyi kuchelewesha kumalizika kwa kesi hiyo kwa sababu za kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *