July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zogo bungeni, wapinzani wafura

Bunge la Tanzania

Spread the love

HATUA ya Bunge la Jamhuri kupitisha Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.5) wa mwaka 2019, imetibua wapinzani. Anaripoti Danson Kaijage
 … (endelea).

Muswada huo umepitishwa huku malalamiko kutoka upinzani yakitawala.

Upinzani imepinga kwa madai, kolamu ya wabunge haikutimia kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Nagima Giba, Mwenyekiti wa Bunge ndiye aliongoza kikao cha bunge wakati wa kuchangia na kupitisha muswada huo leo tarehe 6 Septemba 2019.

Baada ya wabunge kumaliza kuchangia na kutaka bunge likae kama kamati kwa ajili ya kupitisha vifungu, wabunge wa upinzania walidai kuwa akidi haikuwa imetimia.

Ester Bulaya ambaye ni Mbunge wa Bunda, aliomba utaratibu ili kueleza bunge kutokidhi kwa akidi, lakini Giga alimnyima nafasi hiyo.

Wabunge hao walipaza sauti kusisitiza juu ya kutokidhi kwa akidi katika kupitisha miswada huo. Giga aliwapuuza.

Wabunge walisisitiza kuwa wamefanya hesabu na kubaini wabunge waliopo ni 63, hivyo akidi ya wabunge haikuwa imekamilika na kwamba wanavunja kanuni.

Hata hivyo Giga alisema, zipo kamati tatu zote zinafanya kazi na zimejiridhisha kuwa akidi imekamilika.

Hali hiyo ilisababisha zogo kutokana na wapinzani kutoridhika na uamuzi wa Giga.

Hata hivyo, Giga aliwataka wapinzania wanapokuwa wakifanya marekebisho ya sheria, wapate msaada kutoka kwa wanasheria ili kufanya marekebisho kukubalika.

error: Content is protected !!