Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ZLSC yaipeleka ZEC kortini Z’bar
Habari za Siasa

ZLSC yaipeleka ZEC kortini Z’bar

Nyundo ya Hakimu
Spread the love

KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), kimefungua kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, kupinga Sheria ya Uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 10 Oktoba 2019 na Ofisi ya Mawasiliano ya ZLSC, inaeleza kwamba kesi hiyo imefunguliwa Oktoba Mosi mwaka huu na kupewa namba 3/2019.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kesi hiyo imefunguliwa ili Mahakama Kuu ya Zanzibar itoe ufafanuzi juu ya uhalali wa kuwepo kwa kifungu cha 143 cha Sheria ya Uchaguzi Nambari 4 ya mwaka 2018, ambacho kinazungumzia uwezo na mamlaka ya jumla ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kituo hicho kinadai kuwa, kifungu hicho kinaeleza tume itakua na uwezo, jukumu na mamlaka katika kuamua jambo lolote linalohusiana na uchaguzi, ambalo halikuwekewa masharti katika sheria na uamuzi wake utakuwa wa mwisho na hautahojiwa na mamlaka yoyote.

“Kituo kimeamua kufungua Shauri la Kikatiba katika Mahakama Kuu ya Zanzibar. lengo na madhumuni ya ZLSC ni kutafuta ufafanuzi wa Mahakama Kuu juu ya uhalali wa kuwepo kwa kifungu hicho,” inaeleza taarifa hiyo na kuongeza ;

“Hivyo kituo kimeona kwamba, iko haja ya kupata ufafanuzi na tafsiri ya kifungu hicho cha 143 katika Mahakama Kuu ya Zanzibar ambayo ni mahakama ya kumbukumbu kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 93 (1) cha Katiba ya Zanzibar (1984).”

ZLSC kimeeleza kwamba, kwa mara ya kwanza kesi hiti imetajwa mahakamani hapo, leo tarehe 1 Oktoba 2019

“Kituo kinafanya hivyo ili kuhakikisha sheria haziendi kinyume na katiba sambamba na kuzingatia misingi ya demokrasia na haki za binadamu,” inaeleza taarifa ya kituo hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!