August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ziwa Victoria kutumika kilimo cha umwagiliaji

Ziwa Victoria

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema inafanya tathimini katika mikoa yote inayolizunguka Ziwa Victoria ili kuanza ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano tarehe 8 Juni, 2022 na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akizungumza na wananchi wa Kata ya Bwanga mkoani Geita kwenye msafara wa Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea mkoani Geita.

“Nataka kuwahikikishia wanachato , Geita, Mwanza, Simiyu, Mara na Kagera tunafanya ‘visibility study’ Ziwa Victoria ili tuanze ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.”

Aidha amesema katika Mkoa wa Geita wanatangaza miradi minne ya umwagiliaji yenye jumla ya hekta 3,400 katika maeneo ya Ibanda, Igongwa, Chato masasi , Bukombe Nyampambwe, na kwamba watatumia mtindo wa usanifu na ujezi ili wananchi waweze kulima mwaka mzima.

Amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha inaondoa changamoto za wakulima ikiwemo kutoa zuruku za mbolea ili kushusha bei.

“Kuanzia mwaka ujao tunatoa zuruku ya mbolea ili kushusha bei na wakulima waweze kutumia mbolea ya kutosha,” amesema Bashe.

Katika hatu anyingine Bashe amesema Wilaya ya Chato ni moja ya wilaya zinazolima pamba na hapa zao lilikufa pamoja na kiwanda.

“Mwaka huu na mwaka jana tuliwapa mbegu bure na dawa bure na leo wameanza kulima pamba,” amesema.

Bashe ameongeza kuwa bei elekezi ya pamba iliyotolew ana Serikali ni 1,560 kwa kilo moja, “lakini leo bei imefika 1,700 hadi 1,900 na hizi ni fedha ukienda kuuza pamba bei ya ushirika hutakiwi kukatwa hela ya dawa wala hela mbegu.”

error: Content is protected !!