April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto, Wakili wa Serikali wamuibua Azory mahakamani

Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amedai kuwa amefurahi kumsikia wakili wa Serikali anakiri kuwa Mwandishi wa habari za uchunguzi, Azory Gwanda amefariki. Anaripoti Mwanandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameibuka leo tarehe 18 Machi 2020, wakati Zitto akijitetea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele Hakimu Mkazi Huruma Shaidi. 

Zitto akihojiwa na Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali Mwandamizi.

Katuga amemhoji Zitto juu kauli yake lengo la kufanya mkutano wa vyombo vya habari amejibu kuwa lengo ni kuishikiniza Serikali na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi juu matukio yaliyotokea Mpeta.

Katuga amemuuliza Zitto Juu ya njia za kufikia ujumbe kwa serikali akajibu miongoni mwanzo ni kupitia vyombo vya habari.

Zitto alipoulizwa kwa namna gani wananchi walihusika kwenye ujumbe huo ikiwa alilenga Serikali na jeshi la Polisi liufanyie uchunguzi amejibu kwa mujibu wa katiba Serikali ni ya wananchi hivyo nao wanawajibu wa kupata taarifa.

Wakili wa Serikali alimuuliza Zitto kwanini anashtakiwa kwa kutoa maneno ya uongo akajibu hakushtakiwa kwa kusema maneno ya uongo isipokuwa ameshtakiwa kwa uchochezi ndipo Wakili Katuga akamuuliza kwanini asishtakiwe kwa kueleza habari za kifo cha Ben Saanane au Azory Gwanda Zitto akajibu “Mheshimiwa Hakimu Nimefurahi kusikia Wakili wa Serikali amesema kuwa kweli Azory Gwanda amefariki.

 

error: Content is protected !!