Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Wabunge ‘makasuku’ wanatukwamisha Bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Zitto: Wabunge ‘makasuku’ wanatukwamisha Bungeni

Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo ameeleza kuwa wingi wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bungeni kuna kwamisha maslahi ya wananchi kutokana kutumia wingi wao kupitisha yanayowapendeza watawala. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Ofisi za Chama cha CHAUMA akiambatana na viongozi wa vyama kumi vya upinzani vilivyoungana kutetea demokrasia na kupinga muswada wa sharia ya vyama vya siasa.

Vyama hivyo ni pamoja na ACT-Wazalendo, Chama cha Wananchi (CUF) Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi, NRD, CCK, CHAUMA.

Zitto amesema kuwa muswada wa sheria ya vyombo vya habari utapelekwa bungeni ambapo wabunge wa CCM ambao ndiyo wengi bunge watawashinda wabunge wachache wa upinzani na kupelekea kupita kwa sheria hiyo ya vyama vya siasa ambayo wanaiona ni sheria shetani na ovu kwa demokrasia.

“Bunge limejaa wabunge wa CCM, kuna wabunge wazuri wa chama cha mapinduzi lakini kuna wabunge ‘makasuku’ kiasi kwamba muswada huu ukienda utatoka mbaya zaidi,” amesema Zitto na kuongeza.

“Kuna wabunge wapenda sifa wataufanya muswada huu kuwa mbaya zaidi na tayari tuansikia wapo wabunge watakaopendekeza kwenye sharia hiyo kwamba hakuna kufanya mikutano mpaka uchaguzi hadi uchaguzi.”

Zitto ameeleza kuwa muswada huo uliolenga kuua demokrasia ya kweli ambapo Msajili wa vyama vya siasa atakuwa na mamlaka kamili juu kuingilia mambo ya ndani ya vyama vya siasa.

“Toka ilipoingia madarakani serikali ya awamu ya tano imejipambanua vyema isivyokuwa muumini wa demokrasia, Katiba na hata sheria za nchi yetu, imekuwa serikali inayoongozwa na matamko na kauli kana kwamba nchi iliyotoka vitani

“Itakumbukwa tamko la kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara lilitolewa na Rais John Magufuli wakati anahutubia wanachama wa CCM Mkoani Singida mwaka 2016, tamko hilo lilikuwa kinyume cha katiba na sheria za nchi ambapo linaendelea kushikiwa bango na vyombo ya ulinzi na usalama kwa kuwabana wapinzani wakati chama tawala kikiendelea na shughuli zake za kisiasa mahali popote bila pingamizi,” amesema Zitto.

Zitto ameeleza kuwa wakati vyama vya siasa vya upinzani vikipingana na agizo na tamko hilo lililokinyume cha sheria na katiba na chungu kwao Serikali imepeleka bungeni Muswada wa sheria itakayohalalisha tamko hilo.

Hata hivyo tayari vyama hivyo vikiwakilishwa na Zitto, Joran Bashange na Salim Bimani wamefungua kesi kwenye Mahakama Kuu ya kupinga kupelekwa kwa muswada huo bungeni.

Shauri hilo namba 31 la mwaka 2018 litakaloanza kusikilizwa kesho tarehe 4 Januari 2019 mbele ya jopo la majaji watatu.

Shauri hilo lilifunguliwa 20 Desemba mwaka 2018 kwa hati ya dharura tarehe, walalamikaji wanawakilishwa na wakili Mpare Mpoki na Daimu Halfani na mlalamikiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!