July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto ampa ushauri mgumu Rais Magufuli

Spread the love

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Rais John Magufuli kuhakikisha matokeo ya visiwani Zanzibar yanatangazwa haraka ili kulinda amani ya nchi. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

ACT-Wazalendo wametoa maoni yao juu ya sintofahamu ikiendelea visiwani Zanzibar baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta matokeo yote ya uchaguzi.

Hayo ameyasema leo wakati mkutano wa viongozi wa chama hicho na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya chama jijini Dar es Salaam.

Zito amesema kwa maoni ya chama cha ACT-Wazalendo baada ya kupitia sheria ya Zanzibar kinaona kuwa hadi sasa Zanzibar haina serikali, rais wala makamu wa rais kwa sababu kikomo cha Rais aliyekuwa madarakani kimeshafika tayari.

Amesema mtu yeyote anayesema kuwa yeye ni Rais wa Zanzibar atakuwa amepindua na kukiuka miiko ya sheria kwani kikomo cha rais aliyekuwa madarakani kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein kilikuwa ni Novemba 2 ambapo alitakiwa kutangazwa rais mpya.

Zito ambaye pia ndiye mbunge mteule pekee kupitia chama cha ACT-Wazalendo, aliyeteuliwa kuwa mbunge wa Kigoma Mjini katika uchaguzi wa mwaka huu amesema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania hivyo ni vyema ikaangaliwa hasa katika kipindi hiki kigumu cha kusubiri rais mpya kwani kuna badhi ya mambo yanafanyika bila ya kufuata sheria.

Amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha hakuwa na mamlaka ya kufuta uchaguzi badara yake wajumbe wanne, tume pamoja na mwenyekiti ndio wenye mamlaka kwa kukaa pamoja na kufuta uchaguzi.

“Kama imeshindikana kutangazwa matokeo basi rais wa muungano atangaze hali ya hatari Zanzibar,” amesema Zitto.

error: Content is protected !!