June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto: Tunamuheshimu Afande Sele

Spread the love

CHAMA chetu kitalinda na kuheshimu mawazo ya Selemani Msindi (Afande Sele) ingawa wengine hawatopendezwa na hili, anaandika Wolfram Mwalongo.

Ni kauli ya Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa twitter akijibu mashambulizi ya Afande Sele, aliyekuwa mgombea ubunge wa chama hicho katika Jimbo la Morogoro mjini kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Jana Afande Sele aliandika kwenye ukurasa wake wa Istagram ujumbe uliowatuhumu viongozi wa ACT-Wazalendo.

“Labda hatuelewi au hatujielewi. Wakati wa kampeni walimshambulia Lowassa (Edward Lowassa, mgombea urais kupitia Chadema) na uchaguzi ulipoisha walimpongeza rais (Rais John Magufuli) na kujipendekeza mpaka wakampa ilani ya chama chetu akaitumie akiwa Ikulu….

“Leo tumegeuka, Kiongozi Mkuu (Zitto Kabwe) kila siku anamponda Magufuli na chama chake halafu kiongozi mwingine ndani ya chama anamponda Lowassa sijui wanachama tusimamie wapi!”  ameandika Afande Sele.

Kwenye mtandao huo Zitto amesema, kila mtu anao uhuru wa kutoa mawazo yake ingawa wapo ambao hawatapendezewa nayo lakini chama kinapaswa kuheshimu.

Aidha, kiongozi huyo ameahidi kuyafanyia kazi ambapo ametumia nafasi hiyo kutupa kijembe kwa vyama vinavyo fukuza wanachama wake ambao hutoa dukuduku pale wanapo ona mambo hayaendi sawa.

“Inawezekana watu wasipende maoni ya afandesele lakini uhuru wake wa kutoa mawazo yake utalindwa kwa nguvu zote…

“Maoni ya afandesele tunayaheshimu na tutayafanyia Kazi. Sisi sio Kama vyama vingine ambapo Wanachama wakitoa maoni WANAFUKUZWA,” ameandika Zitto

 

error: Content is protected !!