Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Sikuona mambo haya serikali zilizopita
Habari za SiasaTangulizi

Zitto: Sikuona mambo haya serikali zilizopita

Marais wastaafu wa Tanzania
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo amedai kuwa, katika tawala za marais watatu waliopita, hakuwahi kuona mambo yanayofanyika kwenye serikali ya sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amedai, kwenye serikali hizo zilizopita – uongozi wa Alhaj Ali Hassani Mwinyi, Rais Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete, hakukuwa na ulaghai kwa wananchi kama ilivyo sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Juni 2019, kwenye ofisi ndogo za ACT-Wazalendo, Magomeni jijini Dar es Salaam Zitto amesema, sekali ya sasa kila mwaka inaeleza kuwa na nia njema ambayo haionekani.

“Katika umri wangu huu, nikiwa na akili timamu angalau nimeweza kuona uongozi wa awali ya pili ya Rais Mwinyi (Alhaj Ali Hassani Mwinyi), miaka yote 10 ya Rais Mkapa (Benjamin Mkapa) na miaka yote 10 ya Rais Kikwete (Jakaya Kikwete), sijawahi kuona serikali ambayo inaongoza kulaghai Watanzania kama serikali hii,” amesema na kuongeza;

“Njia ya kuzimu imejaa nia njema, kwa mtu ni rahisi kusema nina nia njema kumbe chini ya ile nia njema kumejaa nia ovu kubwa. Huwezi kusema una nia njema mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu na mwaka wa nne.”

Akieleza kuyumba kwa uchumi wan chi Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa, serikali imeshindwa kuimarisha ustawi wa uchumi wa nchi  licha ya kuwajaza wananchi matumaini.

Na kwamba, kuna tatizo ambalo linaikabili uongozi wa sasa kutokana na kubadilisha mawaziri na watendaji wengine mara kwa mara.

“Mimi na Maalimu Seif (Maalim Seif Shariff Hamad) siku moja tulikuwa tunajadiliana, akaniambia kitu ambacho viongozi wengi hukisema `The Back Stops here’…huwezi kila wakati wewe unapeleka lawama kwa wasaidizi wako tu kila siku…”

Kiongozi huyo amesema, ni muda kwa Watanzania kufanya uamuzi juu ya serikali ya awamu ya tano katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye chaguzi.

“…Ni muda kwa Watanzania kutafakari, kama mtu tuliyempa kutuongoza anafaa, uamuzi ni wa Watanzania wenyewe kwenye sanduku la kura.

“… na sio mbali, tuendelee kuvumilia mwakani Oktoba inafika, tukabidhi nchi kwa watu wanaoweza kuendesha uchumi vizuri na wanaweza kulinda misingi ya demokrasi,” amesema Zitto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!