Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Shilingi ya Tanzania shakani
Habari za SiasaTangulizi

Zitto: Shilingi ya Tanzania shakani

Noti za Elfu Kumi
Spread the love

KUYUMBA kwa uzalishaji na uuzaji wa zao la korosho nchini katika msimu wa korosho wa 2018/2019, kunatajwa kuweza kuporomosha thamani ya Shilingi ya Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hadi sasa minada takribani mitatu katika msimu huu wa korosho iliyofanyika kuanzia Oktoba 22 hadi 24, 2018, imegonga mwamba kutokana na wakulima kugoma kuuza korosho zao kufuatia kutoridhishwa na bei zilizofikiwa na kampuni katika minada hiyo.

Miongoni mwa sababu za wakulima kugoma ni kwamba, bei zilizotajwa na kampuni hizo kutolingani na gharama za uzalishaji.

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia akaunti yake ya Twitter leo tarehe 25 Oktoba 2018 ameandika kuwa, kukwama kwa uuzaji wa korosho msimu huu, kunaweza kukateteresha Shilingi ya Tanzania.

“Kadhia ya zao la Korosho sio suala la bei tu, ni uzalishaji pia. Uzalishaji unakadiriwa kuporomoka kwa 40% mwaka huu kwa sababu ya pembejeo kama sulpher kuchelewa kuwafikia wakulima baada ya Serikali kukwapua/kunyakua pesa za Ushuru wa Korosho. Korosho ITATETERESHA TZS,” ameandika Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini.

Mnada wa korosho katika msimu wa 2018/19 umezinduliwa rasmi Tarehe 22 Oktoba mwaka huu, huku tatizo la bei likiwa kikwako kikubwa kwa wakulima kuuza korosho. Katika mnada huo, bei ya juu ilikua Tsh 2717 na chini ikiwa Tsh 1711.

Kwenye mnada wa pili ulioendeshwa na Chama cha wakulima wa Mtwara na Masasi na Nanyumu (MAMCU) uliofanyika Wilayani Nanyumbu tarehe 23 Oktoba 2018,  Wakulima waligoma kuuza Korosho zao kutokana na bei ya juu kuporomoka hadi Tsh 2520 kwa kilo na ya chini Tsh 2000, ikilinganishwa na bei ya mnada wa kwanza ambayo ilikua Tsh.1711 hadi Tsh.2717.

Baada ya Minada miwili ya mwanzo kugonga mwamba kufuatia wakulima Kugoma kuuza korosho zao kwa kutoridhishwa na Bei ya Tsh. 2717(mnada wa kwanza) na 2520(wa pili), mnada wa tatu uliofanyika jana Oktoba 24 2018, ulioendeshwa na  Chama Cha Wakulima wa Korosho Wilaya za Ruangwa Nachingwe na Liwale(RUNALI) pia ulikwama.

Mnada huo wa tatu ulikwama baada ya bei ya korosho kutoridhisha wakulima, ambapo bei ya juu ilikuwa Tsh. 2657 na ya chini ikiwa Tsh. 2200.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!