December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto: Nilimwombea mama asife hadi aone naapishwa kuwa Rais

Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)

Spread the love

 

KIONGOZI wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameoneshwa shahuku na ndoto aliyonayo ya kuwa Rais wa Tanzania, baada kusimulia alivyokuwa akimfariji mama yake kuwa hatofariki hadi aone anaapishwa kuwa Rais. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Zitto ambaye amewahi kuwa mbunge wa Kigoma Mjini, amesimulia mkasa huo leo Jumapili tarehe 30, Oktoba, 2022 wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu ya chama chake.

Amesema katika kumfariji mama yake ambaye hivi sasa ni mrehemu, alimtakia maneno hayo na kuongez akuwa angetamani angalau mama yake angeshuhudia uzinduzi wa ofisi hizo zilizopo Magomeni Mtaa wa Mbweni.

“Wenzangu huwa mnaa wasiwasi sana ninapopanda kwenye majukwaa ya kisiasa wanasema niko emotional na kweli leo nipo emotional na nahisi naweza hata nikakufuru nitaomba Mungu anisamehe,” amesema Zitto.

“Mama yangu alipokuwa mgonjwa, limtia moyo kuwa hutakufa atasubiri uone nikiapishwa kuwa Rais lakini alikufa na leo nikawa najiuliza kwanini hakusubiri hata aone hili,” amesema Zitto

error: Content is protected !!