Monday , 29 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Zitto, Nape, Polepole wafika na ujumbe msibani kwa Dk. Mengi
Habari Mchanganyiko

Zitto, Nape, Polepole wafika na ujumbe msibani kwa Dk. Mengi

Spread the love

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, wamekutana nyumbani kwa Marehemu Dk. Reginald Abraham Mengi na kutoa salamu za rambirambi za vyama vyao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwenye msiba huo Polepole amesema, CCM na Tanzania kwa ujumla itaukumbuka mchango wa Dk. Mengi kupitia uwekezaji wake mkubwa alioufanya katika sekta ya viwanda.

Na kwamba, ni wakati muafaka kwa umma wa Watanzania kuyaenzi yale aliyoyafanya mfanyabiashara huyo, ikiwemo kuwa wazalendo wa taifa lao.

“Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, uongozi wake wa taifa, chini ya ndugu John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Katibu wetu Mkuu, ndugu Bashiru Alli Kakulwa, napenda kwa niaba yao kuleta salamu za pole kwa familia ya Mzee Mengi,” amesema Polepole na kuongeza;

“Napenda kuleta salamu za pole kwa familia ya Mzee Mengi, kwa ndugu jamaa na marafiki na wote tulioguswa na msiba huu, tunamkumbuka sana na tutaendelea kuwa hivyo kama Mtanzania mzawa na muwekezaji mkubwa katika sekta ya viwanda, amekuwa na mguso kwa wananchi wengi wa hali zote.”

Kwenye salamu hizo Polepole amesema, wanafahamu kuwa wakati huu ni mgumu na hakuna maneno mazuri sana ya kueleza namna ambavyo Dk. Mengi aligusa mioyo ya Watanzania.

“Tunapenda kusema Bwana alitoa Bwana ametwaa, wito wetu kwa umma tuendelee kuyaishi yale yote mema ambayo Mzee Mengi aliyaishi na aliyapanga kuyaishi kuwa mwema, madhubuti na mfano mwema kwa Watanzania.”

Zitto ambaye pia Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, anafikisha salamu za chama chake kwa familia ya Dk. Mzee na Watanzania walioguswa na msiba huo.

“Kwa niaba ya wanachama wa ACT, pia natoa salamu zangu za pole kwa wafiwa wote kuanzia familia. Pili wafanyakazi na wakurugenzi wa IPP Group, ni rahisi sana kupata muda kuanza kueleza Mzee Mengi alikuwa mtu wa aina gani na kadhalika.

“Ili imeishaelezwa na watu wengi sidhani kama itakuwa busara kuwachosha, itoshe poleni sana tutakuwa pamoja hapa Dar es Salaam na Machame ili kuweza kuwapa moyo wafiwa wote, mke wa marehemu ,watoto na ndugu na jamii.”

Kwenye msiba huo, Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama amesema, mfanyabiashara huyo enzi za uhai wake, alifanikiwa kutumia maisha yake kubadili maisha ya wengine hasa katika kuwainua waliokuwa chini.

“Ninapofikia namna ya kuzungumza maisha yangu na safari ya kisisasa bila kumtaja Mzee Mengi haiwezekani, ni mtu ambaye mchango wake katika maisha yangu ya kisiasa kufika hapa nilipofika ni mkubwa.

“Na hiyo inatufundisha jambo moja tu kwamaba, unaweza ukabadili maisha yako lakini kuyatumia maisha yako kubadili ya wengine ni vigumu.”

Nape amesema, amefika nyumbani kwa Mzee Mengi kusherehekea yake (Dk. Mengi) kwa kuwa, amekuwa na mchango mkubwa wa kubadili maisha ya Watanzania walio wengi.

 “Niko hapa kusherehekea maisha ya baba yangu, mzee wangu mtu ambaye alifanikiwa kubadili maisha yake lakini pia alibadili maisha ya wengine, na mimi Nape ni mfano wa watu ambao maisha ya Mengi yaliathiri maisha yangu na leo nafurahia.

“Watu wengi watazungumza mengi juu ya huyu mzee, lakini wakati wote ni wakati muafaka wa kuyaenzi aliyotufundisha.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

Habari Mchanganyiko

Kampeni ya Samia Legal Aid yazinduliwa Manyara, kesi 45 zapokelewa

Spread the love  KAMPENI ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, imezinduliwa...

Habari Mchanganyiko

NMB ya kwanza kuzindua Malipo kwa QR na UnionPay International

Spread the loveBENKI ya NMB kwa kushirikiana na UnionPay International (UPI), wamezindua...

error: Content is protected !!