Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto, Mrema walilia MAWIO
Habari za SiasaTangulizi

Zitto, Mrema walilia MAWIO

Spread the love

MUDA mfupi baada ya Serikali kutangaza kulifungia gazeti la MAWIO kwa miaka miwili, Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na John Mrema, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi – Chadema wamelaani kitendo hicho, anaandika Charles William.

Katika taarifa yake kwa umma, Zitto amesema kuwa kitendo cha Serikali kulifungia gazeti la MAWIO ni cha uonevu na kinapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia.

Serikali imelifungia gazeti la MAWIO ambalo hutoka kila wiki kwa kile ilichokieleza kuwa ni kutumia picha za Marais wastaafu Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete na kuwahusisha na sakata la mchanga wa makinikia kinyume na agizo la Rais Magufuli.

Zitto amesema, “Hakuna mkataba ulioingiwa bila ridhaa ya Baraza la Mawaziri, Rais Magufuli aliposema kuwa hatapona mtu ni wazi kuwa alikuwa akiwachimba watangulizi wake.

Kila wakati Rais Magufuli analalamika kuhujumiwa na kutaka kuombewa lakini adui wa Rais Magufuli ni Magufuli mwenyewe. serikali ilifungulie MAWIO kwani kulifungia ni kuwanyima Watanzania mawazo mbadala juu ya mambo ya hovyo yanayoendelea nchini.”

Kwa upande wake Mrema amesema, serikali ya awamu ya tano imekuwa ikibana uhuru wa vyombo vya habari kwa kuzuia mambo mbalimbali kujadiliwa ikiwemo sakata la Faru John na sasa kuzuia kujadiliwa kwa marais wastaafu Mkapa na Kikwete.

“Gazeti la MAWIO ni la wiki na linatoka kila Alhamis, lakini huchapishwa Jumanne. Serikali imetangaza zuio siku ya Jumatano ambapo gazeti lilishachapishwa, na bado wanalifungia kwa katazo lilisokuwa la kiserikali kwani halikutangazwa katika gazeti la Serikali,” amesema Mrema.

Mrema amesema kama kweli Rais Magufuli anataka kukabiliana na ufisadi na ubadhirifu hapa nchini basi hana budi kuruhusu vyombo vya habari vifanye uandishi wa habari za uchunguzi ili vimsaidie kubaini yale yaliyofichika.

“Rais hawezi kujua kila kitu yeye peke yake na asiziamini ripoti za Prof. Mruma na Prof. Osora tu. Tabia ya kufungia vyombo vya habari haikubaliki na ninamshangaa waziri wa habari ambaye ni mwanasheria kwa kulifungia gazeti lilitochapishwa kabla ya agizo la serikali,” amesisitiza Mrema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

error: Content is protected !!