Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Zitto, Maalim Seif waeleza machungu ya Rais Magufuli
Tangulizi

Zitto, Maalim Seif waeleza machungu ya Rais Magufuli

Hayati Maalim Seif Sharif Hamad
Spread the love

MTINDO wa uongozi wa Rais John Magufuli, umeelezwa na viongozi wawili wa Chama cha ACT-Wazalendo, kwamba umesababisha machungu kwa Watanzania. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo leo tarehe 31 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam amesema, miaka mine ya uongozi wa Rais Magufuli, imegubikwa na machungu mengi.

“Napenda kutoa pole kwa watu wote ambao wamepata madhila mbalimbali katika kipindi hiki cha mwaka 2019,” amesema Zitto.

Akitaja baadhi ya machungu waliyokumbana nayo Watanzania kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa, ametaja vitendo vya utekaji raia bila hatia, mauaji yanayofanywa na ‘watu wasiojulikana,’ kukamatwa wanaharakati, wanasiasa na wakosoaji wa serikalina wengine kufunguliwa kesi zisizo na dhamana.

“Miaka hii tumeshuhudia misukosuko ya utawalaa huu. Makundi mbalimbali ya jamii yameumizwa na maamuzi na matendo ya watawala ikiwemo wakosoaji, viongozi wa vyama vya siasa mpaka wananchi wa kawaida, wakulima na wafugaji,” amesema Zitto na kuongeza;

“Wakosoaji wa watala wamekumbana na mateso. Wapo waliouawa, walioteketea na kupotea hadi leo hatujui walipo. Wapo waliomiminiwa risasi nje ya Bunge mpaka leo hakuna lililoshughulikiwa, wapo waliolipuliwa ofisi zao na mabomu wako waliobambikiwa kesi ili kuwadhibiti wasiweze kufanya shughuli zao za kawaida.”

Akizungumzia uchumi wan chi, Zitto ambaye ni mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini amezungumzia kufurugwa kwa mifumo ya uchumi wa nchi pamoja na kuongezeka deni la taifa.

“Takwimu zinaonesha…nazao yaliyokuwa nafuu mwaka jana serikali ya Magufuli (Rais) imevuruga. Mbaazi, korosho zilikuwa zinaenda vizuri lakini zimevurugwa, mambo ni hayo hayo kwenye mahindi, tumbaku n.k.”

“Katika maiaka mine tunayoiaga leo, serikali imeongeza deni wastani wa trilioni 4 kila mwaka. Tunapomaliza mwaka, kila Mtanzania anadaiwa  milioni 1.2 wakati mwaka 2015 kila Mtanzania alikuwa anadaiwa 920,000.”

Akizungumzia miaka mine ya utawala wa Rais Magufuli, Maalim Seif Shariff Hamad, Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo amesema, Wazanzibar na Watanzania wameshuhudia ukata katika maisha yao.

Amesema, tatizo la uhaba wa ajira limekomaa, misharaha ya watumishi wa umma imekwama pale pale huku ubaguzi wa kiitikadi  ukishamiri visiwani Zanzibar.

“Kumeibuka ubaguzi katika ajira, utafutaji nyaraka ikiwemo hati za kusafiria, vyeti vya kiaraia na wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu ambapo hutolewa kwa ubaguzi, kwa kutegemea itikadi zao kisiasa. Kuna ubadhirifu mkubwa ulioko serikalini, kila mmoja anamfumbia macho mwenzake.

“Wafanyabiahsra wako hoi kwa kodi kubwa, vijana hawana ajira, mauzo ya nje yameporomoka kutokana na uzalishaji wa zao la mwani kuporomoka hivyo kusababisha kipato cha wananchi wa kawaida kushuka.

Maalim Seif amesema, Zanzibar ambayo kiasili ni nchi ya biashara, imeporomoka kutokana na bandari kutopanuliwa, viwanja vya ndege kutomalizika kwa wakati na utengenezaji wake gharama kupanda sana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kung’oka tena

Spread the loveUWEZEKANO wa Paul Makonda, kuendelea na wadhifa wake wa mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Mabeyo awataje waliotaka kuzuia urais wa Samia

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu...

Habari za SiasaTangulizi

Vilio vyatawala miili ya wanafunzi wanafunzi ikiagwa Arusha

Spread the loveHUZUNI na vilio vimetawala kwa maelfu  ya waombolezaji wakiwemo familia...

error: Content is protected !!