Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto, Maalim Seif na Membe walivyozungumzia ujio wa Lissu
Habari za Siasa

Zitto, Maalim Seif na Membe walivyozungumzia ujio wa Lissu

Benard Membe (kushoto) akiwa na Zitto Kabwe pamoja na Maalim Seif
Spread the love

VIGOGO wa siasa za upinzani nchini Tanzania , Maalim Seif Sharif Hamad, Zitto Kabwe na Bernard Membe wamemkaribisha nchini humo kwa maneno ya faraja Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwenye kuraza zao za twitter, wameeleza kufurahishwa na ujio wake nchini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Lissu aliwasilia jana Jumatatu saa 7 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam akitokea nchini Ubelgiji.

Mwanasiasa huyo amerejea Tanzania baada ya kuwa ughaibuni tangu tarehe 7 Septemba 2017, aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa ndani ya gari katika makazi yake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria kikao cha Bunge.

           Soma zaidi:-

Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo kwenye ukurasa wake wa twitter amesema, ni faraja kwa Lissu kurejea nchini.

“Naungana na Watanzania wenzangu kumkaribisha nyumbani ndugu yangu Lissu. Hakika ni furaha na faraja kubwa kukuona umerudi Tanzania wakati taifa linajiandaa kuandika historia kwa kufanya mabadiliko yatakayohitimisha utawala wa CCM hapa nchini. Tuko pamoja,” ameandika Maalim Seif

Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo ameandika “Tundu Lissu niungane na mamilioni ya Watanzania kukukaribisha Nyumbani.”

“Mapokezi makubwa na ya amani uliyoyapata leo (jana) kutoka kwa wananchi na hasa Chadema ni ushahidi wa upendo kwako na salaam kwa watawala kuwa mitano inatosha! Sasa tujipange na tuunganishe nguvu! Tutashinda!”

Wakati Zitto akiandika hayo, Bernard Membe ambaye amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu huo ujao amesema, makaribisho yake yameonesha upendo walionao Watanzania kwake.

“Tundu Lissu, karibu nyumbani. Umati uliokupokea ni ishara ya mapenzi makubwa kwako na shukrani kwa Mola. Sisi Viongozi wa ACT – Wazalendo na wenzako wa Chadema. Tunahakikisha tutakuwa na ushirikiano madhubuti ili kuleta mabadiliko. Kurejea kwako ni chachu. Ni furaha kubwa kwetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!